Mkuu wa Wilaya ya Urambo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mhe. Elibariki Bajuta amewataka madiwani na Wananchi kushirikiana kuhamasisha suala la lishe bora kwa Watoto Shuleni ili kuhimarisha afya kwa Watoto hao. Ameyasema hayo leo Februari 15, 2024 akizungumzakatika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani ya Halmashauri ya Wilaya Urambo kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya.
Mhe. Bajuta amebainisha suala la utoro kama moja ya changamoto inaendelea kuikabiri wilaya ya Urambo. amesema Utoro bado upo na kuna watoto bado hawajaripoti mpaka sasa na kuwaagiza Watendaji, Madiwani, na Wananchi kwa ujumla kuhakikisha watoto walitakiwa kuripoti shuleni wafike shuleni.
Mhe. Mkuu wa Wilaya amesema Watoto wameandikishwa kwa asilimia 101 na kuvuka lengo lililowekwa licha ya kwamba bado kuna Watoto hawajaripoti shuleni. Na kwamba Mkurugenzi na Wataalamu wake wamefanya kazi kubwa mpaka sasa.
Aidha DC Bajuta amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji (W) Urambo kwakushirikiana na Wakuu wa Idara na Wataalamu wao kutembelea miradi na kuwaelimisha wananchi kujua Miradi inayoendelea kwenye maeneo yao. Na kwamba asilimia kubwa ya miradi inaenda vizuri lak
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa