Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha amefungua Mafunzo ya Maafisa Usafirishaji na Madereva Wakuu wa Taasisi za Umma na Halmashauri Kanda ya Magharibi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Reli, Manispaa ya Tabora.
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Maafisa Usafirishaji na Madereva Wakuu wa Taasisi za Umma na Halmashauri Kanda ya Magharibi.
Baadhi ya Maafisa Usafirishaji na Madereva Wakuu wa Taasisi za Umma na Halmashauri Kanda ya Magharibi wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha akimuwakikisha Mkuu wa Mkoa Wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian.
Mkuu wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji Tanzania (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akitoa ufafanuzi juu ya Mafunzo ya Maafisa Usafirishaji na Madereva Wakuu wa Taasisi za Umma na Halmashauri Kanda ya Magharibi kabla ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha kutoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kwa niaba ya Maafisa Usafirishaji na Madereva Wakuu wa Taasisi za Umma na Halmashauri Kanda ya Magharibi, mmoja ya Maafisa hao Ndugu. Lucy Emily akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasm Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha mara baada ya kutoa hotuba yake.
Mafunzo ya Maafisa Usafirishaji na Madereva Wakuu wa Taasisi za Umma na Halmashauri Kanda ya Magharibi yamefunguliwa leo Oktoba 23, 2023 na yanatarajiwa kufungwa mnamo Oktoba 27, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa