Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt Batilda Salha Burian amewataka Vijana Mkoani Tabora kujipanga na kuchangamkia miiradi mbalimbali kupitia sekta ya Kilimo ambayo Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewekeza fedha nyingi ambazo zimelenga kuwagusa vijana na kuhakikisha Mkoa na Taifa kwa ujumla linakuwa na chakula cha kutosha.
Ameyasema hayo leo alipokuwa akifanya mahojiano kwenye kipindi cha Sentro kinachoruswa na kituo cha Clouds Tv leo Septemba 5, 2023.
Aidha, kupitia Mkutano Mkuu wa Kujadili Mifumo ya Chakula Barani Afrika (African Food System Forum) Mkuu wa mkoa wa Tabora amemshukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa kuhakikisha sekta ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo inagusa vijana na wanawake kwa kiasi kikubwa. Na Kwamba yeye kama kiongozi wa Mkoa atahakikisha miradi mingi ya Kilimo na ufugaji inawagusa Wanawake na Vijana Mkoani Tabora.
“ kupitia program ya Kijana Ongea na Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Tabora alifanikiwa kukutana na vijana wengi ambao walifanikiwa kufahamu fursa mbalimbali zilizopo Mkoani Tabora na Tanzania kwa ujumla ambao kupitia program hiyo ulifanikiwa kupata vijana walioenda kujiunga na program ya BBT ( Build Better Tomorrow)”
Alisema Mkuu wa Mkoa.
Ikumbukwe kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amehudhuria Mkutano Mkuu wa Kujadili Mifumo ya Chakula Barani Afrika (African Food System Forum) wa mwaka 2023 uliofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Philip Mpango, jijini Dar Es Salaam Septemba 5, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa