• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

WAKAZI WA IGUNGA WATAKIWA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Posted on: September 17th, 2019

WAKAZI WA IGUNGA WATAKIWA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

SERIKALI Mkoani Tabora imewataka wakazi wa Igunga kutumia mafunzo mbalimbali wakati wa utekelezaji wa Mradi Shirikishi wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi Igunga (Igunga ECO – Village) katika kuhakikisha waendelea kufanya shughuli ambazo ni rafiki wa mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa sherehe za kufunga Mradi Shirikishi wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Igunga.

Alisema wakiendelea kuzingitia mafunzo waliyopata wataendelea kuwa na uhakika wa chakula wakati wote na kukabiliana na magonjwa mbalimbali ambayo yanatokana na ukosefu wa vyoo safi na salama hasa yale ya mlipuko.

Mwanri alisema kuwa katika kipindi cha minne mradi huo ambao umetumia zaidi ya shilingi bilioni 5 umeweza kutekelezaji shughuli mbalimbali zinahusika na upunguzaji wa athari zamazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Alizitaja shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuwaelimisha wakulima kuongeza uzalishaji mazao . upandaji wa miti, ujenzi wa majiko banifu, uvunaji wa maji ya mfua, ujenzi wa vyoo vya kisasa na ufugaji wa kuku, samaki na ng’ombe.

Mwanri aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kuhakikisha unaendeleza mafunzo hayo katika Kata zote za Wilaya hiyo ili wananchi wengi waweze kupata elimu ya ulizashaji wa mazao ambao ni rafiki na mazingira kwa ajili ya kuwa na chakula kiingi wakati wote.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wakulima wa Kata ya Mbutu na Igunga waliokuwa wakinufaika na mradi wa Igunga Eco Village Mathias Luhende alisema baada ya mafunzo wakulima wa eneo husika wametambua mbinu za kilimo na uvuvi ambao ni rafiki na mazingira.

Alisema pia wameweza kuboresha utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti, usafi wa mazingira kuanzia ngazi za kaya zao, shule  na katika Taasisi za dini kwa kuimarisha ujenzi wa vyoo vya kisasa.

Luhende aliongeza kuwa wamepunguza tatizo la upatikanaji wa maji kwa kujifunza teknolojia ya uvunaji wa maji na uchimbaji wa visima na matumizi ya chujio la maji ambalo limepunguza magonjwa la mlipuko kwenye eneo la mradi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Revoctaus Kuuli alisema mradi huo umesaidia kutoa elimu mbalimbali ikiwemo ufugaji wa samaki ambapo kwa kipindi cha miaka minne cha utekelezaji umeweza kutoa jumla ya vifaranga 90,000 vya samaki ili kuwawezesha kujiongezea kupato na kuepuka kufanya shughuli zinaharibu mazingira.

Alisema kupitia mradi huo wakazi wa Kata hizo wameweza kuunda na kuanzisha  Kamati  49 za usafi na mazingira kwa ajili ya ufuatiliaji wa usafi ngazi ya kaya ili kuikinga jamii na magonjwa ya mlipuko.

Kuuli alisema katika kipindi cha miaka minne ya utekelezaji wa mradi huo jumla ya sola 600 zimetolewa kwa kwa wanafunzi na wakulima na kupata mafunzo ya utengenezaji wa majiko banifu ambapo majiko 58 yalitengenezwa.

Mradi huu ulianza kutekelezwa katika Kata za Mbutu na Igunga wilayani Igunga 2015 na ulihusu sekta za  Mazingira na Maliasili, Maji, Kilimo na Uvuvi na Maendeleo ya Jamii .

Mradi huu ulikuwa ukifadhiliwa na Umoja wa Nchi za Jumuiya ya Ulaya ,Shirika la Mitamba Uholanzi (Heifer Nederland), Shirika la Mitamba (HEIFER Tanzania), Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Fiziolojia ya Wadudu na Mazingira (ICIPE), Maji kwa wote( Aqua for All ) kwa kushirikiana na  Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa