• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

WAKURUGENZI MKOANI TABORA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MIRADI YA ARDHI

Posted on: March 6th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri katika Wilaya zote za mkoa huo kutenga fedha kwa ajili ya sekta ya ardhi katika bajeti ya mwaka 2024/25 ili kuendeleza utekelezaji katika maeneo yale ambayo Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) hautekelezwi.

 

Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema wadau wa ardhi mkoa wa Tabora watumie fursa kujadili namna bora ya kutekeleza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) katika maeneo yao wakiongozwa na kaulimbiu inayosema ‘‘Usawa Wa Kijinsia Katika Umiliki Wa Ardhi Kwa Ustawi Wa Jamii Yetu’’

 

Akifungua mkutano huo Machi 6, 2024 mkoani Tabora, Dkt. Batilda Burian amesema wadau hao wamepata muda mwafaka wa kujadili mwelekeo wa jinsi mradi utakavyotekelezwa na kujadiliana namna bora ya kutatua changamoto zitakazojitokeza klatika halmashauri zao.

 

“Mkutano huu umekuja muda muafaka katika mkoa wetu hasa mwezi huu wa Machi ambao unaenda sanjari na Siku ya Wanawake Duniani yanayoongozwa na kaulimbiu inayosema ‘‘Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii’’ ni ni heshima kubwa mradi huu kutekeleza katika Wilaya zetu” amesema Balozi Dkt. Batilda.

 

Mradi huo unatekelezwa katika mkoa wa Tabora katika halmashauri za Kaliua, Sikonge, Uyui, Urambo, Nzega Mjini, Nzega Vijijini na Manispaa ya Tabora.

 

Mkuu wa Mkoa amesisitizitiza kuwa Mkoa huo upo mstari wa mbele katika kutekeleza mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi kwa maendeleo ya wananchin wa Mkoa huo. 

 

Aidha, Mkuu wa Mkoa  amewataka wataalamu wa sekta ya ardhi washirikiane na viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji kuwapa wananchi elimu kuhusu masuala ya ardhi ili kutoa taarifa sahihi ambazo zitasaidia kurahisisha utekelezaji wa mradi huo.

 

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa LTIP Bw. Joseph Shewiyo amesema mradi huo unalenga kupanga matumizi ya ardhi kwa maendeleo ya vijiji na miji, kuhamasisha umiliki wa ardhi kwa pamoja, kuzingatia haki za makundi maalum katika umiliki wa ardhi pamoja na usawa wa kijinsia katika umiliki wa ardhi.

 

Bw. Shewiyo ameongeza kuwa hadi sasamradi huo umeongeza idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi kutoka asilimia 25 hadi 38 hali inayosaidia kufikia azma ya Serikali ya kuwaletea wananchi usawa wa kijinsia katika umiliki wa ardhi.



Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa