Mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa majengo manne katika hospitali ya wilaya ya Urambo Mkoani Tabora. Akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi huo uliogharimu shilingi milioni 900, kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023 Ndugu, Abdalla Shaib Kaim amesema,
“Mhe. mkuu wa wilaya nikupongeze wewe binafsi ukiwa kama msimamizi wa shughuli za serikali ndani ya wilaya yako ikiwa pia ni pamoja na program mbalimbali za maendeleo, kwa upande wa ujenzi tumekagua, tumetembelea, tumehakiki vipimo pamoja na kuangalia ubora wa mradi huu itoshe kusema mhe. mkuu wa wilaya viwango na ubora vimezingatiwa”
Kwa niaba ya Wananchi Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Magret Sitta amemshukuru Dkt. Samia kwa kutoa fedha nyingi katika sekta ya Afya, na kwamba maboresho haya yatapunguza changamoto katika hospitali hiyo. Pia ametoa pongezi kwa uongozi wa Wilaya kwa kusimamia vema mradi huo wenye tija kwa wananchi wa Urambo.
Mradi huu wa Ujenzi wa Majengo Manne (4) ni miongoni mwa miradi nane (8) ambayo itapitiwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo. Ambapo Mapema leo Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Kenani Kihongosi aliupokea kutoka Wilaya ya Kaliua
Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Tabora Septemba 14, 2023 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Kiloli, Wilayani Sikonge. ambapo utahitimisha mbio zake ukiwa umezindua jumla ya miradi 50 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 22.2 na kukabidhiwa Mkoa wa Singida Septemba, 21, 2023.
Kauli Mbiu ni "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa