Wajasiriamali zaidi ya arobaini kutoka kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Tabora kuwakilisha Mkoa kwenye maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi kuanzia Disemba 5, 2023 hadi Disemba 15, 2023.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt Batilda Salha Burian wakati wa Uzinduzi wa Ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) mnamo Disemba 2, 2023 alieleza kuwa tayari Mkoa umeshapata wajasiriamali ambao watakwenda nchini Burundi kwenye maonesho ya biashara ya Afrika mashariki ambapo huko bidhaa kutoka Tabora zitauzwa
“Nimeshapokea taarifa kuwa kuna wajasiriamali kutoka Tabora watakwenda nchini Burundi kushiriki kwenye maonesho ya biashara ya Afrika Mashariki ambayo yanatarajiwa kufunguliwa Disema 5, 2023” alisema Mkuu wa Mkoa
Maonesho hayo yanafanyika katika Viwanja vya Cercle Hyppique (Golf Course), Bujumbura yakiongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Kuunganisha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki kufanya biashara katika eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki’.
Baadhi ya wajasirimali kutoka Mkoani Tabora wakiwa tayari kwa safari ya kwenda nchini Burundi.
Baadhi ya wajasiriamali kutoka Mkoani Tabora wakiwa na furaha na bashasha mara baada ya kuingia nchini Burindi kwa kupitia mpaka wa Manyovu, Mkoani Kigoma.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa