• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

ZIARA YA MHE RAIS. DKT SAMIA SULUHU HASSAN MKOANI TABORA

Posted on: October 17th, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili Mkoani Tabora kwa ajili ya ziara yake ya kikazi kwa siku mbili (2) ambapo atakagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mikubwa ya maendeleo na kisha kuwa na mkutano wa hadhara wilayani Igunga na Nzega.

 

Akiwa Wilayani Igunga, Mhe. Rais ameweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa Chuo Cha Veta, na kisha kwenda kuongea na maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa Barafu, Wilayani Igunga. Na akiwa Wilayani Nzega ataweka jiwe la msingi kwenye mradi wa Umwagiliaji (Center Pivot) unaosimamiwa na Wakala wa Mbegu Tanzania (ASA).

 

Akiwa anaelekea Wilayani Nzega, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alifanya mazungumzo na wananchi wa Ziba na kisha kuendelea na ziara yake Wilayani Nzega ambapo alikutana na kufanya mkutano wa hadhara na maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa Samora.

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian mara baada ya kuwasili Wilayani Igunga kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa Chuo Cha Veta uliopo Wilayani Igunga.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa Ndugu. Hassani Wakasuvi mara baada ya kuwasili Wilayani Igunga.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akitazama na kupata burudani ngoma ya kinyamwezi kutoka kikundi cha Wayege mara baada ya kuwasili kwenye Chuo cha Veta, wilayani Igunga.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akicheza wimbo mzuri kutoka Kwaya ya Shule ya Msingi Majengo.

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akiungana na viongozi wengine wa Serikali kuweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Chuo Cha Veta.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi wengine wakikagua madarasa na miundombinu mingine iliyopo kwenye mradi mkubwa wa Chuo cha Veta Wilayani Igunga, mara baada ya kuweka jiwe la msingi.

 

Mamia ya wananchi kutoka Mkoani Tabora waliofika na kumsubiri, kumuona na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye Uwanja wa Barafu Wilayani Igunga.

 

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Salha Burian akitoa salamu za Mkoa kwa Maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mhe. Dkt Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Barafu Wilayani Igunga. 

 

 Akitoa salamu zake, Dkt. Batilda amemshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi ambazo zimetekeleza miradi mingi na mikubwa ya maendeleo Mkoani Tabora ikiwemo ya Afya, Kilimo, Elimu pamoja na biashara na uwekezaji.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akiwahutubia maelfu ya wananchi Wilayani Igunga. Ambapo sehemu kubwa ya hotuba yake Mhe.Rais mafanikio ya Serikali ya awamu sita katika kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inakamilishwa.

 

Rais ameelezea mipango ya Serikali katika kuimarisha Sekta ya Kilimo hususani suala la Ruzuku, maendeleo makubwa yaliofanywa na serikali katika ujenzi wa Vyuo vya Ufundi yaani VETA, ambapo tayari Serikali itahakikisha kila wilaya inakuw ana chuo cha Ufundi ili kutoa nafasi kwa vijana.

 

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Igunga waliojitokeza na kusikiliza hotuba ya Mhe. Dkt Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Barafu uliopo Wilayani Igunga.

 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akiongea na wananchi wa Ziba alipokuwa njiani kuelekea Wilayani Nzega.

  Maelfu ya wananchi kutoka Mkoani Tabora waliofika na kumsubiri, kumuona na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye Uwanja wa Samora Wilayani Nzega.

 

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Salha Burian akitoa salamu za Mkoa kwa Maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mhe. Dkt Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Samora Wilayani Nzega.

 

Akitoa salamu zake, Dkt. Batilda amemshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi ambazo zimetekeleza miradi mingi na mikubwa ya maendeleo Mkoani Tabora ikiwemo ya Afya, Kilimo, Elimu pamoja na biashara na uwekezaji.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akiwahutubia maelfu ya wananchi Wilayani Nzega. Ambapo sehemu kubwa ya hotuba yake Mhe.Rais ameeleza mikaka ya kuwaendeleza vijana kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo (BBT). Pia ameelezea mikakati mbalimbali ya kuendelea Mkoa wa Tabora kupitia fursa mbalimbali zinapatikana Mkoani Tabora. Aidha Mhe. Rais Dkt. Samia ameeleza maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Biashara na Uwekezaji na kuwataka vijana kufanya kazi kwa bidi.

 

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Igunga waliojitokeza na kusikiliza hotuba ya Mhe. Dkt Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Samora Wilayani Nzega.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa