Naibu Waziri wa Maji Mhe. Eng. Maryprisca Mahundi (Mb) amefanya ziara ya siku moja (1) wilayani Urambo na kutembelea mradi wa usambazaji wa maji ya ziwa Victoria awamu ya pili uliofikia asilimia 32 ya ukamilishwaji wake.
Amesema “leo hii tunakagua mradi huu muhimu wa usambazaji wa maji kwa wilaya ya kaliua, urambo na sikonge na niwapongeze masimamizi wote wa mradi huu kwa kazi kubwa wanayofanya kwa ushirikiano mkubwa sana”
Sambamba na hilo Mhe. Naibu Waziri amempongeza Mh. Rais Dkt. Samia kwa kutoa fedha Zaidi ya bilioni 145 kukamilisha mradi huu ambao utakuwa na tija kwa wanaurambo na Tanzania kwa ujumla.
“tunatarajia mpaka kufika mwishoni mwa mwaka huu tayari tutakuwa tunakunywa maji safi na salama kutoa ziwa Victoria” alisema Mhe. Naibu Waziri
Ikumbukwe, Utekelezaji wa Miradi yam aji Mkoani Taboraimeongeza kiwango cha upatikanaji wa Maji safi na salama kwa wakazi waishio Mjini ambao umefikia Asilimia 75 ukilinganisha na lengo la Asilimia 95 na Asilimia 68.1 kwa wakazi waishio Vijijini ulinganisha na lengo la kufikia Asilimia 85 mpaka kufikia mwaka 2025.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa