Katika ziara hiyo, Prosefa Makame Mbarawa ametoa wito kwa wasimamizi wa mradi huo ambao ni TANROAD kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi na kukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa.
“Sina mashaka na mkandarasi kwa maana alishafanya kazi nzuri kwenye miradi mingine ya viwanja vya ndege kama Mwanza na Kigoma, lakini ni muhimu kumsimimamia mkandarasi huyo ili kazi ikamilike kwa wakati na yenye viwango” alisema Profesa Mbarawa.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozoi Dkt. Batilda Salha Burian amemuhakikisha Mhe. Waziri Profesa Mbarawa kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliotolewa na kupendekezwa na wziri huyo kuhakikisha fedha zilizotolewa na serikali zinatumika ipasavyo.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa aliwasili leo mkoani Tabora kwa ajili ya ziara ya siku moja ambapo alitembelea mradi wa ukarabati na uboreshwaji wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Tabora
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa