Leo Novemba 24, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameshiriki kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na (Shirika la Mpango wa Chakula Duniani) WFP, kilichohudhuriwa na wawakilishi kutoka WFP, SEIDA, Wakuu wa Wilaya, wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, wataalam kutoka Halmashauri zote za mkoa wa Tabora na Wadau Wengine wa sekta ya kilimo.
Kupitia kikoa hiko Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka Wakuu wa Wilaya wote ambao wilaya Zao zinapitiwa na miradi hiyo, kuandaa ardhi ukubwa usiopungua hekari 100 ambayo itatumika kutekeleza miradi hiyo.
Aidha Dkt. Batilda ametoa wito kwa vijana Mkoani Tabora kuchangamkia fursa zitakazopatikana kwenye miradi hii ya Kilimo Biashara ili kuwaanda vijana kujiajiri na kuongeza pato la taifa.
Ametoa pongezi kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Kilimo na Wadau wote walipendekeza Mkoa wa Tabora kuwa miongoni mwa mikoa saba ambayo itafaidika na miradi ya Vijana ya Kilimo Biashara.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa na Afisa Mahusiano WFP Ndugu. Neema Nima Sitta wakijadiliana kuhusiana na mtama ambao utakwenda kutumika kwenye miradi mbalimbali ya kilimo itakayokuwa chini ya WFP, wengine ni Mratibu wa Mradi kutoka WFP Ndugu. Abiud Gamba, Mwenyekiti wa Bodi ya SEIDA Ndugu. Edward Mboga, Afisa Mtendaji Mkuu kutoka SEIDA na Katibu Tawala Msaidizi Kilimo na Biashara Ndugu. Bedavenerabilisy Chamatata Novemba 24, 2023
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye mazungumzo na Afisa Mahusiano kutoka WFP Ndugu. Neema Nima Sitta, Mratibu wa Mradi kutoka WFP Ndugu. Abiud Gamba, Mwenyekiti wa Bodi ya SEIDA Ndugu. Edward Mboga, Afisa Mtendaji Mkuu kutoka SEIDA na Katibu Tawala Msaidizi Kilimo na Biashara Ndugu. Bedavenerabilisy Chamatata, waliofika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Novemba 24, 2023
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa Mahusiano (Shirika la Mpango wa Chakula Duniani) WFP Ndugu. Neema Nima Sitta, Mratibu wa Mradi kutoka WFP Ndugu. Abiud Gamba, Mwenyekiti wa Bodi ya SEIDA Ndugu. Edward Mboga, Afisa Mtendaji Mkuu wa SEIDA na Katibu Tawala Msaidizi Kilimo na Biashara Ndugu. Bedavenerabilisy Chamatata. Novemba 24, 2023
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwasili kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na (Shirika la Mpango wa Chakula Duniani) WFP Mkoani Tabora, kinachofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.
Badhi ya Wakuu wa Wilaya kutoka Mkoa wa Tabora wakiwa kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na (Shirika la Mpango wa Chakula Duniani) WFP Mkoani Tabora, kinachofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.
Makatibu Tawala kutoka Wilaya zote Mkoani Tabora wakiwa kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na (Shirika la Mpango wa Chakula Duniani) WFP Mkoani Tabora, kinachofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.
Baadhi ya Wenyeviti wa Halmashauri Mkoani Tabora wakiwa kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na (Shirika la Mpango wa Chakula Duniani) WFP Mkoani Tabora, kinachofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi, Novemba 24, 2023.
Baadhi ya wataalam wa Kilimo na Biashara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora washiriki kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na (Shirika la Mpango wa Chakula Duniani) WFP Mkoani Tabora, kinachofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi, Novemba 24, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akihutubia kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na (Shirika la Mpango wa Chakula) WFP Mkoani Tabora, kinachofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi, Novemba 24, 2023.
Afisa Mahusiano kutoka WFP Ndugu. Neema Nima Sitta akitoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na mradi wa vijana wa Kilimo Biashara unasimamiwa na WFP kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na (Shirika la Mpango wa Chakula) WFP Mkoani Tabora, kinachofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi, Novemba 24, 2023.
Mratibu wa Mradi kutoka WFP Ndugu. Abiud Gamba akitoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na mradi wa vijana wa Kilimo Biashara unasimamiwa na WFP kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na WFP Mkoani Tabora, kinachofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi, Novemba 24, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiongoza majadiliano mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa kuhususiana na mradi wa vijana wa Kilimo Biashara unaosimamiwa na WFP kwenye Kikao cha Kujenga Uelewa wa Pamoja wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara utakaotekelezwa na WFP Mkoani Tabora, kinachofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi, Novemba 24, 2023.
Afisa Mahusiano kutoa (Shirika la Mpango wa Chakula Duniani) WFP Ndugu. Neema Nima Sitta akimkabidhi zawadi ya mkoba Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian.
Mradi wa vijana wa Kilimo Biashara hapa Mkoani Tabora unatarajia kuanza mwa mwaka huu ambapo jumla ya Wilaya tano (5) kufaidika na miradi hiyo zikiwemo wilaya ya Sikonge, Igunga, Nzega, Uyui na Wilaya ya Tabora. Ambapo kati ya wilaya hizo Wilaya nne (Uyui, Nzega, Tabora na Igunga) miradi itajikita kwenye mazao ya Kilimo na wilaya hususani alzeti na mtama. Na Wilaya moja (Sikonge) miradi itajikita kwenye uzalishaji wa asali. Ambapo jumla ya kaya 15,000 kufaidika na miradi hiyo.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa