Katika hatua ya kuimarisha mazingira ya biashara na kuchochea ustawi wauchumi wa wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Mhe. Cornel Lucas Magembe,ameongoza kikao cha Baraza la Biashara Mkoa wa Tabora kwa niaba ya Mkuu waMkoa, Mhe. Paul Chacha. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi mdogo wa ofisi yaMkuu wa Mkoa wa Tabora, kikiwakutanisha wadau kutoka sekta binafsi na za ummakujadili masuala muhimu ya maendeleo ya biashara mkoani humo.
Akifungua kikao hicho, Mhe. Magembe ametoa witokwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanawawezeshawananchi kuandaa maandiko ya miradi na kuyawasilisha kwenye mifuko na programumbalimbali chini ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC). Piaamesisitiza kuimarishwa kwa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi hadi ngaziya kata, kutengwa kwa maeneo ya machinga na kuwezeshwa kwa miundombinu rafiki,pamoja na kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika shughuli zamabaraza ya biashara ili kuinua uchumi wa wilaya husika.
“Kila wilaya inapaswa kuwa na mpango mkakati wa kuimarisha ushirikiano katiya serikali na sekta binafsi. Hili ni jambo la msingi katika kujenga uchumishirikishi na endelevu,” alisema Mhe. Magembe.
Wadau mbalimbali walioshiriki baraza hilowalitumia fursa hiyo kuibua changamoto zinazokwamisha ustawi wa biashara, ikiwani pamoja na ukosefu wa uhusiano mzuri kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na wafanyabiashara, mazingira duni ya kufanyia biashara, pamoja na sheriazisizoakisi hali halisi ya wajasiriamali waliowengi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chemba yaBiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Tabora, Bw. KassongoMirambo, alitoa wito kwa waandaaji wa vikao vya baraza kuhakikisha kuwa wajumbewanapewa mwaliko na nyaraka za kikao mapema ili kuwapa muda wa kujiandaaipasavyo. Alisisitiza umuhimu wa mjadala wa kina unaojikita katika mustakabaliwa biashara na viwanda vya mkoa huo.
Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Bw. Asanterabi Sang’enoi,aliahidi kuwa serikali ya mkoa itafanyia kazi maoni na mapendekezo yoteyaliyowasilishwa na wajumbe wa baraza hilo. Alisema kuwa serikali inalengakuhakikisha kuwa vikao vya baraza vinafanyika kwa wakati katika mamlaka zote zaserikali za mitaa na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha ustawi wa wafanyabiashara.
“Fursa zipo nyingi. Serikali imedhamiria kwadhati kuondoa vikwazo vyote vinavyosababisha usumbufu kwa wafanyabiashara ilikuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa,” alibainisha Bw. Sang’enoi.
Baraza la Biashara Mkoa wa Tabora ni chombohalali kisheria kinachokutana angalau mara moja kwa mwaka kwa lengo la kujadilichangamoto zinazoikabili sekta ya biashara na kuweka mikakati ya kuzitatua,hatua inayolenga kuboresha mazingira ya biashara na kuinua uchumi wa wananchi.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa