Mkuu wa Wilaya ya Urambo Kamishina Mwandamizi wa Uhifadhi Mhe. Eribaliki Bajuta amepokea hundi ya shilingi milioni ishirini na zaidi kutoka Chama Kikuu cha Ushirika Milambo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto ya madawati wilayani Urambo.
Akiongea baada ya kupokea hundi hiyo Mhe. Bajuta alisema kuwa, katika kukabiriana na changamoto ya madawati wilayani hapo kumeanzishaa Kampeni ya ukusanyaji wa madawati inayoitwa “Dawati ni Elimu Kukaa chini Urambo Sasa Basi” yenye malengo ya kukusanya madawati elfu sita mia tano na ishirini (6520), na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangia madawati hayo.
Aidha, Mhe. DC amebainisha kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa madawati ambapo tayari wameshaanza kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kikiwemo Chama Kikuu cha Ushirika Milambo, ili kuona nmna sahihi ya kukabiria na changamoto hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya (W) Urambo Ndugu. Grace Quintine amesema kuwa fedha hizo zilizopokelewa zinakwenda kutengeneza madawati zaidi ya mia Tisa (900) ambapo halmashauri na wadau wengine wakichangia kutapatikana madawati si chini ya elfu mbili (2000).
Mrajisi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora Ndugu. Venance Msafiri amesema kuwa, vyama vya Msingi vinaongozwa na misingi mikuu saba (7) na moja ya misingi hiyo ni hii ya utoaji wa fedha kwa halmashauri husika. Na ofisi yake imehaidi kuweka mikakati kuhakikisha vyama vya msingi vinagusa jamii moja kwa moja kupitia utoaji wa misaada kwa jamaii.
Naye, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Milambo Ndugu. John Ntezilyo ameleza kwamba, wataendelea kuboresha mazingira mazuri ya wanafunzi kwa kutambua jitihada za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha sekta ya elimu nchi na mkoa wa Tabora kwa ujumla.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa