Leo Oktoba 24, 2023, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Nzega na Hospitali ya Rufaa ya Nkinga na kuwajulia hali majeruhi, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza ndugu na jamaa zao kwenye ajali ya basi na lori iliyotokea Oktoba 21, 2023, kata ya Uchama, Wilayani Nzega.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa Hospitali ya Wilaya ya Nzega akiongea na baadhi ya Ndugu na Jamaa wanaosubiri kusafirisha miili ya ndugu na jamaa zao waliopoteza maisha kwenye ajali ya basi na roli iliyotokea Oktoba 21, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwafikisha salamu za pole kutoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa baadhi ya wajeruhi waliopata ajali ya Basi na Lori Oktoba 21, 2023 Kata ya Uchama Wilayani Nzega.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akitoa mkono wa pole na kuwajulia hali baadhi ya majeruhi wa ajali ya Basi na Lori kwa kuwapatia kiasi kidogo cha fedha na Asali kwa ajili ya kutibu majeraha waliyoyapata.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwasili Hospitali ya Rufaa ya Nkinga iliyopo Wilayani Igunga, kwa ajili ya kuwaona na kuwajulia hali Majeruhi wa ajali ya basi wanaoendelea na matibabu hospitalini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiongea na vyombo vya habari alivyoambata navyo, ambapo sehemu kubwa amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhimarisha miundombinu ya Afya, Wilayani Igunga na Nzega ambayo imesaidia kutoa huduma za dharura kwa baadhi ya majeruhi.
Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amewahakikishia majeruhi wote, kwamba Serikali imehakikisha majeruhi wanapatiwa matibabu kwa uharaka na umakini wa hali ya juu, na gharama zote zitalipwa na Serikali kwa kushirikiana na mmiliki wa mabasi wa kampuni ya Alfa.
Pia Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi kwa madaktari, wauguzi na watendaji wa Serikali pamoja na Jeshi la Polisi waliojitoa na kuhakikisha wanaokoa maisha ya watanzania waliopata ajali. Bila kusahau wananchi na Vyombo vya habaroi vilivyotumia muda usiku na mchana kuhabarisha Umma kuhusiana na ajali hiyo mbaya iliopoteza maisha ya watanzania wenzetu.
Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa, mpaka sasa kati ya majeruhi 60 waliofikishwa hospitalini hapo, wamebaki 19 na wote wanaendelea vizuri na madaktari wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanapata unafuu. Kuna majeruhi wawili wapo Bugando nao pia wanaendelea vizuri.
Aidha kwenye ajali hiyo watu 18 walipoteza maisha papo hapo, na miili 13 tayari imekwishatambuliwa na tayari imeshachukuliwa na wanandugu, na mpaka sasa bado miili 5 ambayo tunaendelea kuwatafuta ndugu na jamaa zao ili kuhakikisha waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo wanasitiriwa.
Ikumbukwe kuwa, majira ya saa 5 asubuhi Oktoba 21, 2023 Kata ya Uchama, Wilayani Nzega majira ya saa 5 asubuhi Oktoba 21, 2023 kulitokea ajali iliyohusisha Basi la Abiria, Kampuni ya Alfa lenye namba ya usajili T 612 CQD na Lori la mafuta, Kampuni ya GBP lenye namba ya usajili T.526 AEB na kusababisha vifo 18 na majeruhi 60 ambao wote walifanikiwa kupata matibabu.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa