• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

DKT. MBOYA AFUNGUA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA TASAF AWAMU YA TATU, ATOA PONGEZI KWA UTEKELEZAJI MZURI

Posted on: May 29th, 2025

Na. Mwandishi Wetu – Tabora.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya, amefungua  kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF Awamu ya Tatu – TASAF III), kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mtemi Isike Mwanakiyungi, katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Dkt. Mboya aliwapongeza wataalamu wa TASAF kutoka halmashauri zote za mkoa kwa juhudi na weledi waliouonesha katika utekelezaji wa awamu ya tatu ya mpango huo, akieleza kuwa kazi yao imechangia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo ya mpango wa kupunguza umaskini kwa walengwa.

"Mnatekeleza mpango huu kwa bidii na weledi wa hali ya juu. Mmewezesha kufikiwa kwa malengo yaliyowekwa, niwaombe muendelee na moyo huo wa kuwahudumia Wananchi hususan Kaya Maskini," alisisitiza Dkt. Mboya.

Aidha, alifafanua namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoendelea kuthibitisha dhamira yake ya dhati kwa wananchi kwa kupeleka fedha za kutosha kutekeleza shughuli mbalimbali za TASAF. Tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 2015, mafanikio makubwa yameripotiwa, hususan katika kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025, ambapo jumla ya kaya 41,604 katika vijiji 721 na mitaa 153 mkoani Tabora zimenufaika na mpango huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika kikao hicho, zaidi ya Shilingi bilioni 8.08 zimehawilishwa moja kwa moja kwa walengwa katika kipindi hicho, fedha ambazo zimeleta tija na mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi wa Tabora.

Katika mawasilisho kutoka kwa waratibu wa TASAF wa halmashauri mbalimbali, imebainika kuwa utekelezaji wa mpango huo umeleta mafanikio makubwa katika maeneo mengi ya mkoa kwa kuimarisha maisha ya watu, kuongeza fursa za ajira na kuinua shughuli za kiuchumi za kijamii.

Miongoni mwa maazimio ya kikao hicho ni pamoja na kuimarisha zaidi mikakati ya kuwafikia walengwa kwa ufanisi mkubwa ili kuendelea kupunguza umasikini kwa kasi zaidi. Washiriki wa kikao walisisitiza umuhimu wa kuendeleza usimamizi madhubuti na uwazi katika matumizi ya rasilimali zinazotolewa na serikali na wadau wa maendeleo.

Mwisho.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • RAS TABORA AKUTANA NA ASKOFU MSAIDIZI WA JIMBO KUU LA TABORA,ASKOFU BUDUDU;ATOA PONGEZI NA SALAMU ZA SERIKALI

    May 29, 2025
  • DKT. MBOYA AFUNGUA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA TASAF AWAMU YA TATU, ATOA PONGEZI KWA UTEKELEZAJI MZURI

    May 29, 2025
  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa