Na. Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tabora.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Rogath Mboya, leo tarehe 29 Mei 2025 amefanya ziara ya heshima na mazungumzo maalum na Askofu Msaidizi mpya wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Askofu Josaphat Jackson Bududu. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ya Baba Askofu iliyopo ndani ya Kanisa la Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, Manispaa ya Tabora.
Katika mazungumzo hayo ya kirafiki na kimaadili, Dkt. Mboya alimpongeza Baba Askofu Bududu kwa kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Hayati Francisko kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Tabora, uteuzi uliofanyika rasmi tarehe 26 Februari 2025, na kuwekwa wakfu tarehe 25 Mei 2025 na Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa.
"Nakupongeza kwa dhati kwa uteuzi huu mkubwa na wa heshima. Ni ishara ya imani kubwa uliyopewa na Kanisa na tunaamini utatoa mchango mkubwa katika huduma ya kiroho na kijamii kwa wananchi wa Tabora," alisema Dkt. Mboya.
Kwa upande wake, Baba Askofu Josaphat Bududu alitoa shukrani kwa serikali na hususan uongozi wa Mkoa wa Tabora kwa ushirikiano na upendo waliomwonesha tangu uteuzi wake, akiahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa serikali katika kuhakikisha ustawi wa jamii unaimarika kupitia mafundisho na huduma mbalimbali za kanisa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa