Na. Robert Magaka –Tabora.
NaibuKatibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu,Bi. Zuhura Yunus, amefungua rasmi mafunzo maalum ya siku tatu kwa MaafisaTEHAMA na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi,kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa kuwatambua watu wenye ulemavunchini (PD-MIS). Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya JM, mjiniTabora.
Akizungumzawakati wa ufunguzi, Bi. Yunus amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezowatendaji hao kuhusu matumizi ya mfumo wa PD-MIS, ili wanaporejea katika maeneoyao ya kazi waanze mara moja kusajili na kuwaunganisha watu wenye ulemavu nahuduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali.
Ameelezakuwa mfumo huo utawezesha Serikali kupata takwimu sahihi na za wakati kuhusuwatu wenye ulemavu, hivyo kurahisisha utoaji wa huduma stahiki kama vileusajili rasmi, upatikanaji wa vifaa saidizi, mikopo isiyo na riba ya asilimia2, na fursa za ununuzi wa umma kwa makundi maalum.
Awali,akiwakaribisha washiriki wa mafunzo hayo, Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa waTabora, Bw. Abakos Deodatus, alieleza kuwa mafunzo hayo yataleta mapinduzimakubwa katika sekta ya ustawi wa jamii, kwa kuwa sasa watendaji watawezakupata taarifa muhimu kwa urahisi na ufanisi zaidi wakati wa kuwahudumia watuwenye ulemavu.
NayeMwakilishi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bi. Amina Mfaki, ameishukuruSerikali kwa kubuni mfumo huo muhimu, na kusisitiza kuwa ofisi yake itaendeleakuusimamia kwa ukaribu ili kuhakikisha unatekelezwa kikamilifu na kwa manufaayaliyokusudiwa.
Kwaupande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu kutoka Ofisi yaWaziri Mkuu, Ndg. Rasheed Maftah, alibainisha kuwa mafunzo hayo ni sehemu yautekelezaji wa kitaifa, yakiwa ni ya awamu ya tatu baada ya kufanyika kwamafanikio katika kanda ya ziwa na kanda ya kati.
Kwahatua hii, Tanzania imeandika historia ya kuwa nchi ya kwanza katika ukanda waAfrika Mashariki kuanzisha na kutumia mfumo wa kidijitali kwa ajili ya utambuzina ufuatiliaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya dhamira yaSerikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha hakuna mwananchi anayeachwa nyuma katikamaendeleo.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa