Mjumbe wa Tume Huru ya Taifaya Uchaguzi (INEC), Mhe. Magdalena Rwebangira, amehitimisha rasmi mafunzo yasiku tatu kwa waratibu na wasimamizi wa uchaguzi wa ngazi ya jimbo, akiwaasakuyatumia maaarifa waliyoyapata kwa weledi mkubwa ili kuhakikisha uchaguzi waRais, Wabunge na Madiwani unafanyika kwa ufanisi mkubwa na kwa kuzingatiasheria za nchi.
Akizungumzawakati wa kufunga mafunzo hayo, Mhe. Rwebangira aliwataka wasimamizikuhakikisha wanawafundisha watumishi wa tume walio chini yao kwa umakini na uadilifu,huku wakizingatia sheria, kanuni na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha,aliwakumbusha umuhimu wa kuwasiliana na wananchi kwa uwazi kupitia vyombo vyahabari, lakini akasisitiza kuwa taarifa zozote zinazotolewa lazima wajirishishekwanza na zihakikiwe kabla ya kutangazwa ili kuepusha taharuki kwa wananchi.“Usikurupuke kutoa taarifa, ni vyema ukashirikiana na wenzako kabla yakuzungumza hadharani,” alisisitiza.
Mhe.Rwebangira alikumbusha pia kuwa mara baada ya kula kiapo, kila mmoja wao nimtumishi wa Tume na anapaswa kutunza siri za kazi kwa mujibu wa Kanuni ya 8 yaKanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2025. Alionya kuwakuvujisha taarifa za ndani ni kuvunja sheria na kiapo cha uaminifu.
Katikamafunzo hayo, washiriki walifundishwa kuhusu mabadiliko ya sheria za uchaguzi,taratibu za upigaji kura, usimamizi wa maombi ya kupiga kura nje ya vituo,pamoja na namna ya kutoa taarifa za mapungufu au kasoro za vifaa vya uchaguzipindi vinapopokelewa. Mafunzo yalijumuisha pia maandalizi ya kutoa elimu kwawasimamizi wa kata na watendaji wa vituo vya kupigia kura.
Kupitiamafunzo hayo, Tume inalenga kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 unafanyikakwa njia ya uwazi, ufanisi na kuzingatia misingi ya demokrasia, kwa manufaa yataifa na wananchi wote.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa