Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya, amewapokea wageni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF), wakiongozwa na Bw. Michael Dalali, Mchambuzi Mwandamizi wa Maendeleo kutoka Serikali ya Canada, walipotembelea ofisini kwake kwa ziara ya kikazi.
Lengo la ziara hiyo ni kufuatilia na kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya elimu inayofadhiliwa na Serikali ya Canada kupitia UNICEF, ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa watoto na jamii nzima kwa ujumla.
Katika ziara yao mkoani Tabora, ujumbe huo unatarajiwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa katika wilaya za Kaliua, Sikonge, Uyui pamoja na Manispaa ya Tabora.
Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tabora inatoa shukrani za dhati kwa wadau wote wa maendeleo na inaendelea kuthamini ushirikiano wa wadau hao, hususan Serikali ya Canada na UNICEF, katika juhudi zao za kuboresha sekta ya elimu na kuimarisha ustawi wa watoto katika mkoa wa Tabora.
Top of Form
Bottom of Form
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa