• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

KAMANDA ABWAO AFUNGUA RASMI UMISSETA TABORA, AHIMIZA NIDHAMU NA UZALENDO KWA WANAMICHEZO.

Posted on: June 2nd, 2025

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao, amefungua rasmi mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) kwa mwaka 2025 katika viwanja vya Shule ya Wavulana Tabora, akihimiza nidhamu, uzalendo, na mshikamano miongoni mwa wanamichezo hao.

Akisoma risala ya ufunguzi kwa niaba ya Kamati ya maandalizi ya michezo hiyo, Afisa Elimu Michezo Mkoa wa Tabora, Mwl. Hassan Katuli, alieleza kuwa zaidi ya michezo saba itashindaniwa katika mashindano hayo, ikiwemo mpira wa miguu, pete, wavu, kikapu, mikono, riadha pamoja na sanaa za maonesho.

Mashindano haya yanahusisha Halmashauri zote nane za Mkoa wa Tabora, yakiwa yamevutia jumla ya washiriki 960 — wasichana 509 na wavulana 451. Aidha, wanamichezo hao wameandamana na timu ya walimu wa michezo, walezi, na madaktari wapatao 144 (wanaume 111 na wanawake 33).

Akitoa salamu za Mkoa, Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Elimu, Bi. Upendo Rweyemamu, alisisitiza kuwa lengo kuu la mashindano haya ni kubaini vipaji bora vitakavyoiwakilisha Tabora katika mashindano ya kitaifa yatakayofanyika mkoani Iringa kuanzia tarehe 18 hadi 30 Juni, 2025. Aliongeza kuwa nidhamu ni msingi mkuu wa mashindano haya na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka taratibu.

Akihutubia hadhira, Kamanda Abwao alitoa shukrani kwa wadau wote waliowezesha kufanikisha mashindano hayo, akitambua mchango wao wa hali na mali. Alieleza kuwa michezo imeendelea kuwa kichocheo muhimu cha fursa, ikiwemo ajira, kuimarisha afya ya mwili na akili, kukuza moyo wa uzalendo na kuleta mshikamano wa kitaifa.

Hata hivyo, alibainisha changamoto kadhaa zinazokwamisha ustawi wa michezo shuleni, zikiwemo uhaba wa vifaa, bajeti ndogo, na mwamko hafifu kutoka kwa wazazi na walezi. Alitoa rai kwa wadau mbalimbali wa michezo, wazazi, na watendaji wa elimu kutambua umuhimu wa michezo na sanaa katika maendeleo ya kijamii na kitaaluma.

“Naomba wadau wote wa michezo Mkoa wa Tabora kuendelea kuchangia maendeleo ya michezo yetu. Wazazi, waone umuhimu wa michezo kwa watoto wenu na wawaruhusu kushiriki kikamilifu. Watendaji katika shule zetu hakikisheni masomo ya michezo na sanaa yanapewa kipaumbele,” alisema Kamanda Abwao.

Aidha, aliwahimiza wanamichezo kuonesha juhudi na nidhamu ya hali ya juu, huku akitoa wito kwa waamuzi kutenda haki ili kusaidia kupatikana kwa timu bora ya Mkoa wa Tabora. Alimalizia kwa kuwahakikishia usalama wa kutosha kwa washiriki wote wakati wa mashindano hayo.

Mashindano haya yanasimamiwa kwa pamoja na Wizara ya TAMISEMI, Elimu pamoja na Utamaduni, Sanaa na Michezo, yakibeba kauli mbiu ya mwaka huu:
“Viongozi Bora ni Msingi wa Maendeleo ya Taaluma, Sanaa na Michezo — Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu.”

Mwisho.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI - JUNI 5, 2025.

    June 04, 2025
  • SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 26.9 KUWAINUA WAKULIMA KUPITIA MRADI WA UMWAGILIAJI MWAMAPULI – IGUNGA

    June 03, 2025
  • KAMANDA ABWAO AFUNGUA RASMI UMISSETA TABORA, AHIMIZA NIDHAMU NA UZALENDO KWA WANAMICHEZO.

    June 02, 2025
  • "SIKU YA WAUGUZI DUNIANI, RAS TABORA ASISITIZA MAADILI, USTAWI NA UWAJIBIKAJI."

    May 30, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa