• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

KOPENI KWA MALENGO YA KUJIPATIA MAENDELE-DAS UYUI

Posted on: May 13th, 2019


KOPENI KWA MALENGO YA KUJIPATIA MAENDELE-DAS UYUI

SERIKALI ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora imewatahadharisha wakazi wa vijiji vya Miyenze na Lutende kutokopa fedha katika Taasisi za fedha bila malengo kwa ajili ya  kuepuka kunyang’anywa ardhi zao baada ya kushindwa kulipa madeni.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Uyui Moses Pesha  wakati wa kufunga mafunzo ya kujengewa uwezo wakulima  100 na viongozi 10 wa Kijiji cha Lutende na kukabidhiwa hati miliki za kimila.

Alisema Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) umeletea neema kwao ni vema wanapotaka kutumia hati zao kukopa iwe kwa kazi maalumu  na sio kukopa kopa ovyo ovyo bila kuwa na mipango mizuri ya kutumia fedha watakazokopeshwa kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

“Hakikisheni mnapokopa iwe kwa ajili ya kazi maalumu na sio kwa ajili ya starehe , anasa na kununua mavazi na urembo…unapokopa hakikisha unalipa deni kwani usipolipa deni  hati hizo zitakuwa sio za kwenu tena hivyo mashamba yenu yatachukuliwa na Taasisi zilizowakopesha” alisema.

Pesha alisema sio vizuri mmoja wa wanafamilia akafanya siri wakati wa kwenda kukopa huku wenzake hawajui, kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha mgogoro baina yao na kufanya kuendelea kuisha kimasikini.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Wilaya ya Uyui amewaonya wakazi wa Vijiji hivyo waliopatiwa hati miliki za kimila baada ya ardhi kupimwa kuepuka kuuza ovyo maeneo yao kwa kuwa wanaweza kusababu kuwa na maskini na kurudisha migogoro.

Alisema mwananchi anapotaka kuuza ardhi ni vema awe na sababu ya msingi na  pia katika kuuza lazima afuate taratibu na sharia zilizopo ili kuepuka kujiingiza katika umaskini.

Pesha aliongeza kuwa hata wanapouziana ni vema wafuate utaratibu wakati wa ubadilishani hati ili kuepuka migogoro baina ya mnununuzi na wanafamilia katika siku za baadae.

Naye Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema mafunzo waliotoa kwa wakazi wa Kijiji cha Lutende na Miyenze katika Wilaya ya Uyui yamewajengea  uwezo wakulima wote waliopata hati ili waweze kutumia mtaji huo  kuboresha ufugaji wa mifugo ikiwemo kuku wa kienyeji.

Alisema pia wanapewa elimu ili waboreshe kilimo , utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za kilimo na biashara na uandishi wa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya uchumi kwa ajili ya uboreshaji wa uchumi wao na wilaya kwa ujumla.

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa