Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika Mkoa wa Tabora yanaendelea kwa mafanikio makubwa, ambapo kamati ya usimamizi wa uchaguzi imethibitisha kukamilika kwa maandalizi yote muhimu. Mahema na vituo vya kupigia kura vimeandaliwa ipasavyo katika wilaya zote za mkoa huo, huku vifaa vya uchaguzi vikiwa vimeshawasili na kuhifadhiwa kwa usalama. Aidha, maafisa wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wao wamepatiwa mafunzo maalum kuhakikisha zoezi linafanyika kwa uwazi, amani na ufanisi.
Msimamizi wa Uchaguzi Mkoa wa Tabora, Elihuruma Nyella, akiwa katika zoezi la ukaguzi wa maandalizi ya vituo vya kupigia kura, amepongeza kazi nzuri inayofanywa na timu ya maandalizi. Amesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba mkoa uko tayari kikamilifu kwa ajili ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumatano, Oktoba 29, 2025, ambapo vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
Wananchi wote wa Mkoa wa Tabora wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura, huku makundi maalum kama wazee, wajawazito, wanaonyonyesha na watu wenye ulemavu wakipewa kipaumbele bila kulazimika kupanga foleni.
Serikali imetoa rai kwa wananchi kudumisha amani na mshikamano katika kipindi chote cha uchaguzi ili kuhakikisha mchakato unakamilika kwa amani na utulivu.
"Kura yako Hahi yako, Jitokeze Kupiga Kura."
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa