• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MAMAKINDA AWATAKA WATANZANIA KUSHIRIKI SENSA IJAYO MWEZI AGOSTI MWAKANI

Posted on: August 4th, 2021

WATANZANIA  na wageni  wote wametakiwa kujitokeza kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi mwezi Agosti mwakani katika tarehe itakayopangwa kwa ajili ya kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi zitakazoiwezesha kupanga mipango ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anna Makinda alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani akiwa katika ziara ya kuangalia mandalizi ya zoezi hilo kubwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Katika siku hiyo Watanzania wote na wasafiri wote na wakimbizi wote watakuwepo katika eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watahesabiwa” amesisitiza.

Makinda amesema sensa ya watu na makazi ijayo itafanyika kitaalamu zaidi kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA ikwemo matumizi vishikwambi( tablets) wakati wa zoezi la kuheshabu watu na hivyo kupunguza matumizi ya karatasi.

Ameongeza kuwa zoezi hilo litakuwa tofauti na awamu za Sensa ya watu na makazi zilizopita kwa kuwa safari hii itafanyika hadi ngazi ya vitongoji kwa maeneo ya vijijini na mijini kwenye Mitaa.

Makinda amesema kwa Mitaa kwa kuwa watakuwa wengi watapangwa kwa kundi la  watu 50.

Amesema sensa ijayo itatoa picha halisi ya idadi ya wananchi waliopo  na kuwezesha Serikali kupanga mipango yake ya maendeleo kwa wananchi vizuri ikiwemo kuepuka suala la kukimbizana kila mwaka katika suala la upungufu wa madawati na huduma nyingine za kijamii.

Aidha Kamisaa huyo wa Sensa ya Watu na Makazi ameuagiza uongozi wa Mkoa huo wa Tabora kutumia vyombo vya habari na zikiwe Redio zinapatikana mkoani humo katika utoaji elimu na kuhamasisha jamii ili watu wote wajitokea hapo mwakani katika kushiriki zoezi hilo muhimu.

Amesema ni vema vyombo vya habari visaidie kutoa elimu kwa jamii kuwa sensa ya watu na makazi haina upande wote wala itikadi yoyote.

Makinda amesema watu wanatakiwa kuona ni ufahari kuwa sehemu ya watu watakahesabiwa hapo mwakani mwezi Agosti katika tarehe itakayopangwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema Mkoa wa Tabora tayari umeshaunda Kamati ya Sensa ya watu na Makazi ya Mkoa na kutoa majukumu kwa kila Mjumbe.

Sensa ya watu na makazi ya mwakani itakuwa ya sita kufanyika  hapa nchini tangu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzishwa 1964 na imekuwa ikifanyika kila baada ya miaka 10.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa