• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MILIONI 416.2 ZAUNGA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI KATIKA SEKTA YA ELIMU NA AFYA

Posted on: May 18th, 2020

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imetoa jumla ya shilingi milioni 416.2 ili kuunga mkono juhudi za jamii katika shughuli za maendeleo ya sekta ya elimu na afya katika mwaka huu wa fedha.

Fedha hizo zimetolewa baada ya kuona mwitiko mkubwa wa wananchi wa kuunga mkono mpango wa Halmashauri wa elimu ya kujiegemea katika kuleta maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa  na Mkurugenzi Mendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima wakati akitoa mada kuhusu umuhimu wa elimu ya kujitegemea katika kuharakisha maendeleo katika mafunzo ya siku mbili ya waajiriwa wapya.

Alisema kati ya fedha hizo Halmashauri hiyo imenunua mabati  Bando 300 za bati kwa gharama ya  shilingi milioni  82.3, saruji mifuko 2,400 kwa  milioni 36.6 na mbao 2,072 za shilingi milioni  7.2 .

Mkurugenzi huyo Mtendaji aliongeza kuunga mkono elimu ya msingi walitoa milioni 15 na sekondari milioni 45 na katika ujenzi wa miundombinu ya afya shilingi milioni 230.

Dkt. Pima alisema baada ya uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kusisitiza umuhimu wa elimu ya kujitegemea kwa wananchi kumekuwepo na mwitiko mkubwa kutoka katika jamii ambao umewapelekea kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya.

Alisema katika kutambua umuhimu wa elimu ya kujiegemea ndani ya mwaka wa fedha huu wazazi katika shule za Msingi wameweza kufyatua matofali zaidi ya milioni 1.9 na kujenga vyumba vya madarasa 93, matundu ya vyoo 69 na nyumba za walimu 11.

Dkt. Pima alisema wanafunzi wameweza kulima mashamba ya mazao mbalimbali kama vile Korosho ekari 118,mahindi ekari 143, alizeti ekari 16,viazi ekari 41, Karanga ekari 80 na Mpunga ekari 23

Alisema kwa upande wa Sekondari jamii imeweza kufyatua tofali zaidi ya laki sita na kujenga vyumba vya madarasa 56, matundu ya vyoo 36,  ya mazao ekari 121,ufugaji mbalimbali,ekari 15 za Korosho; Miti ya mbao ekari 71.8, matunda ekari 5 na mti ya vivuli miche 2,467.

Dkt. Pima alisema katika mwaka ujao wa fedha wanatarajia kuwa na miradi ya kilimo kwa ajili ya chakula,miradi wa Kilimo kwa ajili ya biashara, upandaji miti kila shule na miradi ya matofali kila shule.

Akifunga mafunzo hayo ya siku mbili Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama aliupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kuamua kutekeleza kwa viendo dhana ya elimu ya kujitegemea.

Alisema matokeo yake yameonyesha kuwa kupitia elimu ya kujiegemea Halmashauri zinaweza kuwa na miradi ambayo inawaingizia kipato na kuondokana na kuegemea ruzuku toka Serikali kuu.

Busalama alisema kuwa Halmashauri inaweza kujenga majengo kwa ajili ya viwanda na kupangisha wawekezaji na kupata kodi na kuondokana kutegemea zaidi kodi ya mazao.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa