Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Ndugu, Abdallah Shaibu leo Septemba 15, 2023 amezindua mradi wa Huduma ya Kuchuja Damu unaopatikana katika Hospitali ya Malolo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, wenye thamani ya Shilingi Bilioni moja ambao utaweza kuhudumia wagonjwa 48 kwa siku. Maradi huo umekamilika kwa asilimia mia moja na upo tayari kuto huduma kwa wananchi.
Akiongea na wananchi baada kuzindua mradi huo, Ndugu Abdallah Shaimu aliwapongeza viongozi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora kwa kusimamia vema mradi huo ambao Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa fedha nyingi kukamilisha mradi huu.
Ndugu Abdallah Shaibu Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huu kwakuwa umefuata taratibu zote muhimu ikiwepo maandalizi mazuri ya nyaraka mbalimbali pamoja na vifaa maalumu vya upimaji wa Ubora.
Aidha amewakumbusha wananchi kuwa Serikali ina dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha wananchi wote wanapata elimu yenye viwango na ubora wa hali ya juu.
Mradi huu ni moja ya miradi sita (6) ambayo imezinduliwa hapa Wilayani Tabora na Mwenge wa Uhuru mwaka 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa