Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Matiko Chacha, amefanya ziara yakutembelea mgodi wa Kitunda uliopo wilayani Sikonge, pamoja na kusikilizachangamoto zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.
Akiwasilisha changamoto zinazowakabiliwachimbaji madini wa mgodi huo, Bw. Godfrey Mwaniwiti, Katibu wa Chama chaWachimbaji Madini Mkoa wa Tabora (Taborema), amebainisha kuwa wachimbaji haowanakutana na changamoto ya ukosefu wa mashine ya kisasa ya kuchoronga madini,jambo linalowafanya wachimbaji hao kufanya kazi kwa kubahatisha, badala yakutumia vifaa bora na vya kisasa.
Akijibu suala la mashine za kuchoronga, Bi.Fatuma Kyando, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tabora, ameeleza kuwa Wizara yaMadini chini ya kampuni ya STAMICO tayari imenunua mashine za kisasa zakuchoronga. Aliongeza kuwa katika awamu ya kwanza, mashine hizo zilisambazwakatika mikoa michache, na mkoa wa Tabora umejumuishwa katika mpango wa awamu yapili wa kuletewa mashine hizo. Wachimbaji wa mkoa huo watahitajika kuchangiagharama kidogo ili kuzitumia mashine hizo pindi zitakapofika.
Katika kujibu kero za wananchi wa Kitunda,Mhe. Chacha amesisitiza kuwa ni marufuku kuendeleza shughuli za uchimbaji wamadini katika eneo la hifadhi la Kululu Inyonga East. Amewataka wananchikubakia kwenye maeneo yaliyotengwa na serikali kwa shughuli hizo.
Aidha, Mhe. Chacha ametoa msaada wa mifuko 100ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la mgodi waKitunda, pamoja na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi.Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Mhe. Cornel Magembe, pia amechangia mifuko mingine50. Lengo la michango hii ni kuboresha miundombinu ya kijamii na kuimarishausalama kwa wananchi wa eneo hilo.
Ziara hii wilayani Sikonge imehitimisha ziara ya kutembelea halmashauri zoteza mkoa wa Tabora kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero zawananchi.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa