• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

NMB BENKI YAMKABIDHI MKUU WA MKOA WA TABORA HUNDI YA SHILINGI MILIONI 374.3

Posted on: October 25th, 2023

Leo Oktoba 25, 2023 Benki ya NMB imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Batilda Salha Burian Hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 374.3 ikiwa ni fidia kwa Wakulima wa Tumbaku 1398 waliokumbwa na janga la Mvua za mawe zilizopata kunyesha mwanzoni mwa mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwasili katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi kuhudhuria hafla ya kukabidhi Hundi ya fidia kwa Wakulima wa Tumbaku walioathirika na mvua za mawe

Baadhi ya viongozi wa Serikali, wawakilishi kutoka vyama vya Msingi (AMCOS) Mkoani Tabora pamoja na wadau wa sekta ya kilimo wakiwa ndani ya Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi kushuhudia hafla ya kukabidhi Hundi ya fidia kwa Wakulima wa Tumbaku walioathirika na mvua za mawe.

Kwa niaba ya Wakulima wa Tumbaku Mkoani Tabora Ndugu, Deoglatias Paulo Mwenyekiti (AMCOS) Mtapenda akitoa neno la Shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian na Watendaji wa Benk ya NMB, wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi ya fidia kwa Wakulima wa Tumbaku walioathirika na mvua za mawe. Oktoba 25,2023

Dkt. Lupilya Emmy Meneja wa Mamlaka ya Bima Tanzania  kanda ya Magharibi akitoa salamu kutoka Benki ya NMB kanda ya Magharibi wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi ya fidia kwa Wakulima wa Tumbaku walioathirika na mvua za mawe. Oktoba 25, 2023. 

Katika salamu zake amemuhakikisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, Benki ya NMB itaendelea kutoa elimu ya Bima ya Mazao kwa wakulima wa Tumbaku ili kuhakikisha Wakulima wa tumbaku wanakabiliana na majanga ya mvua za mawe. 

Ndugu Nsolo Mlozi Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa Benki ya NMB amesema kuwa, maboresho ya miundombinu ya barabara yaliofanywa na Serikali ya Dkt. Samia, Mkoani Tabora yamewavutia Watendaji wa Benki ya NMB kuwekeza fedha nyingi Mkoani humo hususani kwenye Sekta ya Kilimo (Tumbaku)  ambacho kimekuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa taifa. Na tayari Benki ya NMB imeunda kitengo maalumu kitakacho husika na kilimo cha tumbaku peke yake.

Akitoa salamu zake, Ndugu Nsolo Mlozi ameeleza mchango mkubwa wa Serikali ya Awamu ya sita kwa kuhimarisha miundombinu ya barabara ambayo imerahisisha shughuli nyingi za kiuchumi na kilimo kikiwemo. Lakini pia Ndugu Nsolo ameihakikishia Serikali kuwa, Benki ya NMB itahakikisha inashirikiana na wakulima wa Tumbaku hususani katika suala la utolewaji wa elimu ya bima ya mazao.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akihutubia watendaji wa Benki ya NMB pamoja na Wawakilishi kutoka Vyama Vya Msingi  vinavyojumuhisha wakulima wa Tumbaku Mkoani Tabora kwenye hafla ya kukabidhi Hundi ya fidia kwa Wakulima wa Tumbaku walioathirika na mvua za mawe iliyofanyka katika Ukumbi wa Isike Mwana Kiyungi, Oktoba 25, 2023. 

Sehemu kubwa ya hotuba yake, Dkt. Batilda Burian amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapa nafasi wadau mbalimbali kuwekeza kwa wakulima hususani suala la Bima ya Mazao. Sambamba na utengaji wa fedha kwa ajili ya Ruzuku ya mbolea. Pia amewashukuru na kuwapongeza watendaji wote wa Benki ya NMB kwa kusimamia maslahi ya wakulima wa Tumbaku hususani kipindi cha mvua ya Mawe kwa kutoa fidia ya Shilingi Milioni 374.3 na kunufaishi wakulima 1398.

Na pia alitoa wito kwa wakulima wa tumbaku Mkoani Tabora kuchanamkia fursa ya Bima ya Mazao ili kupambana na majanga ya asili hasa mvua za mawe ambazo huaribu zao la tumbaku kwa kiasi kikubwa sana.

Kwa niaba ya Wakulima wa Tumbaku, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amepokea Hundi ya Shilingi Milioni 374.3 kutoka Benki ya NMB kama sehemu ya fidia kwa Wakulima 1398 walioathiriwa na mvua za mawe.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi Hundi ya  Shilingi Milioni 374.3 Ndugu, Deoglatias Paulo Mwenyekiti (AMCOS) Mtapenda  kwa niaba ya Wakulima 1398 walioathiriwa na mvua za mawe.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji kutoka Benki ya NMB mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi Hundi ya fidia kwa Wakulima wa Tumbaku walioathirika na mvua za mawe iliyofanyika leo Oktoba, 25 2023 kwenye Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.





Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa