RC AAGIZA HADI MWISHONI MWA SEPTEMBA HOSPITALI YA WILAYA SIKONGE ITOE HUDUMA MATIBABU ZAIDI
UONGOZI wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kuhakikisha ifikapo mwisho wa Septemba mwaka huu wanaongeza huduma mbalimbali za matibabu katika Hospitali hiyo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon wakati muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali wilayani Sikonge.
Dkt. Sengati alisema ni lazima watoe fedha za kuwalipa mafundi ili waweze kukamilisha shughuli ndogo zilizobaki na hatimaye waweze kuweka vifaa ambayo vitawezesha kupanua wigo wa matibabu kwa wananchi.
Alisema Hospitali teule inayotumika hivi sasa imeshaelemewa kutokana kuwa ilijengwa miaka mingi wakati idadi wa wakazi wa Sikonge ilikuwa ndogo na hivi sasa wameongeza na hivyo kuwalizimu kutaka kupata huduma za matibabu katika hospitali hiyo kubwa.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ambao hawana bima kujiunga na na Mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa ICHF ili kuweza kupata matibabu kutoka ngazi za Zahanati hadi Hospitali za Rufaa za Mikoa kwa kutumia gharama za shilingi 30,000/- kwa mwaka.
Alisema haua hiyo itawasaidia kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu kwa watu sita wa kaya moja.
Dkt. Sengati alisema wananchi wakiwa na afya bora wataweza kushiriki kikamilifu katika katika shughuli za kujiletea maendeleo yao na ujenzi wa uchumi wa nchi kwa ujumla.
Aidha aliwataka wataalamu kuendelea kutoa elimu ili wananchi wengi waweze kujiunga na ICHF iliyoboreshwa.
Mwisho
RC ATAKA SIKONGE KUTENGA ENEO KUBWA LA UWEKEZAJI
MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati ameitaka Halmashauri ya Wilya ya Sikonge kutenga maeneo makubwa na ambayo hayana migogoro kwa ajili ya uwekezaji mkubwa na mdogo.
Alitoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea eneo ambalo Halmashauri hiyo inakusudia kujenga Kiwanda cha kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki wakati muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali wilayani Sikonge.
Alisema ni lazima wawe na mpango wa muda mrefu kutafuta eneo kubwa lililopimwa na ambalo halina migogoro ili Mkoa uwasaidia kuwatafutia wawekezaji mbalimbali ambao watasaidia kujenga viwanda ambavyo vitasaidia kuiendeleza wilaya na Mkoa kwa ujumla.
“Mtafute maeneo ambayo hata mwekezaji akija hawezi kukutana na watu kuvamilia eneo lake na wakati mwingine kuharibu mali zake” alisema.
Alisema kuwa Hekta nne walizotenga hazitoshi pindi wawekezaji wakubwa wakitokeza kutaka kuwekeza, hivyo ni vema wakaongeza eneo ili kupata eneo kubwa la uwekezaji.
Dkt.Sengati alisema uongozi wa Mkoa unaendelea na jitihada za kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi ili kuwavutia wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda ambavyo vitasaidia kuupandisha kiuchumi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri alisema wamepanga kuongeza eneo na kufikisha Hekta 500 kwa ajili ya uwekezaji.
Alisema juhudi mbalimbali zinaendelea za kuyaanisha kwa ajili ya kulipa fidia wamiliki wake.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Gadi Mwatebela alisema baada ya andiko la mradi kupitia ,Mfuko wa Mistu Tanzania umetoa udhibitisho wa fedha za ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki.
Alisema Kiwanda hicho kitagharimu shilingi milioni 757.5 ambapo Mfuko wa Mistu Tanzania unatarajia kutoa milioni 719.7 na Halmashauri itachangia shilingi milioni 37.8
mwisho
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa