• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC AONGOZA WAKAZI WA KIJIJI IGOMBE MANISPAA YA TABORA KUADHIMISHA MIAKA 59 YA UHURU KWA KUPANDA MITI ZAIDI 300

Posted on: December 10th, 2020

MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati amewaongoza wanakijiji cha Igombe kilichopo Manispaa ya Tabora kupanda miti zaidi ya 300 ikiwa ni sehemu ya  kuadhimisha miaka 59 ya uhuru wa Tanzania bara.

Zoezi hilo limefanyika  katika eneo la Mistu ya Hifadhi ya Bwawa la Igombe ambacho ni miongoni mwa vyanzo vya maji ya Bwawa la Igombe ambalo litaoa huduma ya maji katika Manispaa ya Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Sengati aliendesha zoezi hilo  ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 59 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

Akizungumza baada ya kupanda miti kwenye eneo hilo la Hifadhi ambalo liloathiriwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo , uchomaji mkaa na ufugaji aliwataka viongozi wa Wilaya zote kuhakikisha wanafikisha lengo la Kitaifa la kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka.

Alisema Ofisi yake itahakikisha inafuatilia ili kupata takwimu sahihi na ikibainika kuwa ipo Wilaya ambayo hakufikia lengo la Kitaifa , hatasita kuwachukulia hatua viongozi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Wakala wa Mistu Tanzania kwa kushirikiana na Mamalaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira Tabora , Manispaa ya Tabora , Bonde la Tanganyika na wananchi katika kulinda na kuhakikisha usalama wa Hifadhi ya Mistu ya Igombe kwa ajili ya kuwahakikisha wakazi wa Manispaa ya Tabora uendelevu wa upatikanaji wa maji kutoka Chanzo cha Bwawa la Igombe.

Aliwataka wadau mbalimbali wanaosimamia uhifadhi wa Msitu huo kuendelea kutoa elimu kwa wakazi wanaozunguka maeneo ya Hifadhi ya Msitu huo kuendelea kuulinda na kuwaondoa wavamizi kwa kuzingatia misingi ya Sheria na taratibu.

Katika hatua nyingine Dkt. Sengati alisema wakati wa zoezi la  upandaji wa miti ni vema wakapanda miti ya miembe na mikorosho ili pamoja na kulinda mazingira waweze kupata kipato kutokana na uuzaji wa maembe na korosho.

Alisema mpango wa Mkoa ni kuanzisha mashamba makubwa ya miembe na mikorosha katika eneo la Tura wilayani uyui kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji wa viwanda vya kushindika matunda kuchukua na kuanzisha viwanda mkoani humo.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Abrahaman Mdeme alisema katika msimu wa mwaka 2019/20 , Mkoa wa Tabora ulipanda miti laki 7.3 na iliyopona ni laki 4.5 .

Alitaja sababu zilizopelekea miti mingi kutopona ni pamoja na kushambuliwa na mifugo, kuchomwa moto , ukame na baadhi ya wananchi kupanda miti kipindi cha mwisho wa msimu wa mvua.

Mhifadhi wa Mistu wa Mnaispaa ya Tabora Peter Kisanga alisema Msitu wa Hifadhi wa Bwawa la Igombe una ukubwa wa Hekta 7,501 ni chanzo maji katika Bwawa la Igombe ambalo ndio linatoa huduma kwa wakazi wa Manispaa ya Tabora.

Alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakivamia Msitu huo wa hifadhi kwa ajili ya shughuli mbalimbali ya kujitafutia kipato kinyume na Sheria zinazoulinda.

Kisanga aliuomba Uongozi wa Mkoa na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Tabora kushirikiana nao katika kuwaondoa watu ambao wamekuwa wakihatarisha uendelevu wa msitu huo na Bwawa la Igombe kwa kuendelea kilimo katika maeneo ambayo hayatakiwi, uvuvi haramu na ukataji wa magogo na uchomaji wa mkaa.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • KAMANDA ABWAO AFUNGUA RASMI UMISSETA TABORA, AHIMIZA NIDHAMU NA UZALENDO KWA WANAMICHEZO.

    June 02, 2025
  • "SIKU YA WAUGUZI DUNIANI, RAS TABORA ASISITIZA MAADILI, USTAWI NA UWAJIBIKAJI."

    May 30, 2025
  • RAS TABORA AKUTANA NA ASKOFU MSAIDIZI WA JIMBO KUU LA TABORA,ASKOFU BUDUDU;ATOA PONGEZI NA SALAMU ZA SERIKALI

    May 29, 2025
  • DKT. MBOYA AFUNGUA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA TASAF AWAMU YA TATU, ATOA PONGEZI KWA UTEKELEZAJI MZURI

    May 29, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa