• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC ATAKA WANANCHI WASHIRIKISHWE KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: May 7th, 2021


RC ATAKA WANANCHI WASHIRIKISHWE KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO


MKUU  wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati ametoa wito kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega na maeneo mengine kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza tija.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuilinda dhidi ya uhujuma yoyote kwa sababu wao watakuwa sehemu ya waliofanikisha kukamilika kwa mradi kutokana michango ambayo watakuwa wametoa.

Dkt. Sengati alitoa kauli hiyo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakati wa ukaguzi wa miradi mitatu ambayo ni ujenzi wa Bweni la wasichana katika Sekondari ya Mwanahala, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwenye shule ya Msingi Uhemeli na ujenzi wa vyumba viwili katika Sekondari ya Kampala.

Alisema wananchi wakielimishwa na kuhamasisha kushiriki katia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao watawezesha kutekelezwa kwa miradi mingi kwa fedha ambayo inaletwa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kiwango kizuri.

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwanahala Agatha Mwaliwale alisema kuwa walipokea kiasi cha shilingi milioni 80 toka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana 80 ikiwa ni mkakati wa kuanzisha cha tano na Sita katika shule hiyo.

Alisema ujenzi umefikia asilimia 95 na wamekwisha tumia kaisi cha shilingi milioni 79.5 na kubakiza shilingi milioni 420.

Agatha alisema kutoka na fedha iliyobaki haiwezi kukamilisha ujenzi , Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imetenga kiasi cha shilingi milioni 20 katika bajeti ijayo kwa ajili ya shughuli zilizobaki.

Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Kampala , Emmanuel Majebele alisema walipokea kiasi cha shilingi milioni 46.6  ambazo zimekabilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matano ya vyoo.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kumesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi na kutoa mazingira mazuri ya kufundisha na kujifunzia.

Katika hatua nyingine Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhemeli Stella Silutongwe alisema walipokea kiasi cha shilingi milioni 47.6  na Halmashauri kuongeza kiasi ya milioni moja ambazo zimekabilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matano ya vyoo na chumba maalumu choo kwa ajili watoto wa kike.

Alisema baada ya kukamika kwa mradi kuwapa nafuu walimu na wananfunzi ambapo hapo awali walilizimika kufundisha kwa awamu mbili kila siku kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

 

 

 

MWISHO

 

 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa