• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC AWATAKA WALIMU WAKUU KUJENGA UMOJA KWA WALIMU WALIOCHINI YAO

Posted on: December 30th, 2020

MKUU wa Tabora Dkt. Philemon Sengati amewataka Walimu Wakuu kuepuka kujenga makundi miongoni mwa walimu wanaowongoza ili kuwafanya kujiona kitu kimoja na kufanyakazi kwa bidii.

Hatua itasaidia kuwa na ushirikiano ambao utaongeza juhudi katika ufundishaji wanafunzi na kuwawezesha kuongoza katika mitihani mbalimbali ya Kitaifa.

Dkt. Sengati alitoa kauli hiyo  mjini Tabora wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule Msingi Tanzania(TAPSHA)  uliokuwa ukijadili mambo mbalimbali ikiwemo mapambano dhidi ya mimba, utoro, rushwa katika mitihani na mbinu za kuongeza ufaulu kwa wanafunzi katika mitihani ya kitaifa.

Alisema walimu wakuu ni lazima wahakikishe wanaweka mazingira mazuri na kuwaongoza  vizuri walimu waliochini yao ili waweze kufanyakazi kwa bidii na moyo wa uzalendo katika kufundisha kwa ajili ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi na kuufanya Mkoa wa Tabora kuwa sehemu ya maeneo mengine nchini kuja kujifunza mbinu bora za ufundishaji.

"Hatutasita kuwachukulia hatua walimu wakuu ambao wanawagawa walimu nakusababisha shule zao kuwa na ufaulu hafifu na kuufanya Mkoa kushika namba za chini...Walimu Wakuu wanatakiwa kuwa mfano mzuri wa uongozi kwa waliochini yao, wale watakaoshindwa kuongoza wenzao kwa misingi ya umoja na mshikamano , tutawaondoa katika nafasi zao na kuwapa ambao watatusaidia kuufanya Mkoa wetu uwe darasa" alisitiza

Dkt. Sengati aliwataka Walimu Wakuu kuendelea kuwachukulia hatua kali baadhi ya walimu wasio waadilifu na wenye tabia mbaya za kujihusisha kimapenzi na wanafunzi na hivyo kuwasababishia kurudi nyuma kitaaluma na wengine wao kukatiza masomo kwa kupata ujauzito.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliwaagiza Walimu Wakuu kuendelea kusimamia ujenzi wa miundombinu ya shule kwa kusingatia matumizi sahihi ya fedha za umma ili kuondoa tatizo la upungufu katika maeneo yao.

Aliongeza walimu Wakuu wanatakiwa kuendelea kuchukua hatua wazazi wa watoto watoro kwa kushirikiana na viongozi wa Kijiji na Kata kwa kuwafikisha katika vyombo vya Sheria ili kutoa fundisho kwa wazazi wengine wenye tabia za kuacha watoto wao nyumba bila kuwahimiza kwenda Shule.

Awali Katibu Tawala Msaidizi anyeshughulikia Elimu Mkoa wa Tabora Michael Ligola aliwataka Walimu Wakuu kuwa na vipindi katika madarasa yanayokuwa na mitihani ya kitaifa kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za walimu wanaofundisha madarasa hayo na kuwatia moyo wanafunzi ili waweze kusoma kwa bidii na kuweza kufaulu kwa wastani wa juu.

Aliongeza sanjari na ufundishaji ni vema wanafunzi wakapewa mazoezi ya kutosha na mara kwa mara kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwa tayari kufanya mitihani mbalimbali ikiwemo ya kitaifa bila woga na hivyo kuweza kufaulu vizuri.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa