Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameshiriki kwenye kikao cha tathmini ya nusu mwaka cha mkataba wa lishe ngazi ya mkoa kilichofanyika katika ukumbi mdogo uliopo ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Tabora leo Februari 29, 2024.
Akitoa hotuba yake, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewata wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wataalamu wote ngazi ya halmashauri kuhakikisha suala la lishe linatiliwa mkazo ili kufikia malengo ya serikali katika kuhimarisha lishe kwa wananchi sambamba na utoaji wa takwimu sahihi za kaya zisizokuwa na choo.
RC Batilda amewapongeza viongozi na watalaamu wote kwa kupambana kikamilifu na ugonjwa wa kipindupindu na kufanikiwa kumaliza ugonjwa huo ambao ulikuwa tishia kwa ustawi wa jamii na kusisitiza suala la usafi kuwa ni ajenda ya kudumu kwa halmashauri zote.
Aidha, Mhe. Batilda amezitaka halmashauri zote kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya utoaji wa huduma ya lishe ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kikamilifu. Na kutoa wito kwa viongozi hao kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa amesema kuwa malengo ya kikao hiko ni kufanya tathmini wa maazimio, maelekezo na maagizo ya kikao kilichopita ambacho kilichofanyika Julai 28, 2023 ili kuangalia maendeleo ya lishe mkoa wa Tabora kwa kuangalia mafaniko na changamoto za ukalishwaji wa lishe.
Kwa upande wa wadau wa afya, Mkurugenzi wa mradi wa Bright, Nutritional International Ndugu. Raphael Katebalila amesema kuwa, taasisi yake kupitia miradi ya lishe ni moja ya mkakati wa taasisi hiyo kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika kuhimarisha lishe kwa wakazi wa tabora.
Ikumbukwe kuwa, vikao vya tathmini ya lishe hufanyika mara mbili (2) kwa mwaka kwa ngazi ya mkoa na hufanyika mara nne (4) kwa ngazi ya halmashauri na malengo makuu ya vikao hivyo ni kuhamasisha suala la lishe kuanzia ngazi ya taifa, kata hadi vijiji.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa