Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Matiko Chacha amewataka viongozi na watendaji mkoani Tabora kufanya kazi kwa bidii kwa kuimarisha umoja na ushirikiani ili kuhakikisha wanatabora na watanzania kwa ujumla wanahudumiwa ipasavyo. Ameyasema haya leo alipokuwa akiongea na viongozi na watendaji mbalimbali kwenye mkutano maalumu wa kumkaribisha mkuu wa mkoa huyo uliofanyika katika ukumbi mdogo ulipo ofisi kwa mkuu wa mkoa wa Tabora.
Sambamba na hilo, Mh. Paul Chacha amewataka watendaji na viongozi mbalimbali kuwajibika katika nafasi zao kwa lengo la kutatua kero mbalimbali zinazojitokea .
Kwa niaba ya wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Tabora Mhe. Sauda Mtondoo amemkaribisha mkuu wa mkoa wa Tabora na kumuahidi ushirikiano kutoka kwa wakuu wa wilaya wote waliopo mkoani Tabora.
Naye Mbunge wa Jimbo la Igalila Mhe. Venant Protas amesema mkoa wa Tabora una majimbo kumi na mbili (12) ambayo yanategemea ushirikiano kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora, na hivyo kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Tabora wanahaidi kutoa ushirikiano katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa kipindi chote.
Mhe. Paul Matiko Chacha anachukua nafasi ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, mara baada ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kuhamishiwa kikazi mkoani Tanga.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa