• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA AAGIZA KUKAMATWA KWA WANAOTUMIA VYANDARUA KINYUME CHA UTARATIBU WA KUJIKINGA NA MBU

Posted on: March 9th, 2020

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaagiza viongozi wa vijiji na mitaa kuwamata watu wote watakutwa wakitumia vyandarua kwa matumizi mengine kando ya kujikinga na mbu.

Alisema matumizi ya vyandarua nje ya kujikinga na mbu yanapingana na juhudi za Serikali za kupambana malaria na kusababisha kupoteza nguvu kazi ya Taifa

Mwanri alitoa kauli hiyo  wilayani Kaliua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi.

Alisema kuwa katika baadhi ya watu wanatumia vyandarua kuvulia samaki katika madimbwi na wengine wanatumia kuzungushia vifaranga vya kuku vishismbuliwe na mwewe.

Mwanri aliongeza kuwa kuna watu wengine wanatumia vyandarua hivyo kwa ajili ya kuzungushia bustani za matunda na mboga mboga ili kuzuia wadudu waharibifu.

Alisema matumizi hayo ambayo ni kinyume cha kujikinga na mbu ni marufuku mkoani na atakayekuwa atachukuliwa hatua.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatatinisibwa alisema mwelekeo wa Serikali ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 ugonjwa wa malaria uwe umetokomezwa.

Alisema takwimu zinaonyesha kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa Mkoa wa Tabora bado ni tatizo ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ina asilimia 16.7 , kufuatia Uyui asilimia 16.1 na Sikonge ambayo ina asilimia 13.9.

Dkt. Rutatatinisibwa alisema Urambo ina asilimia 12.8, Manispaa ya Tabora asilimia 8.9, Halamashauri ya wilaya ya Nzega asimilia 8.7, Nzega Mji asilimia 6.8 na Igunga asilimia 5.6.

Alisema nguvu zaidi zinahitajika katika kupmbana na tatizo la malaria mkoani Tabora.

 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa