MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amezitaka Taasisi za Utafiti wa wadudu kuchunguza matumizi ya salfa (sulfur) wakati wa kunyunyuzia mikorosho kama haina athari kwenye ufugaji nyuki.
Alisema ni kundi makundi ya nyuki yasije yakapotea kutokana na matumizi ya viwatilifu ikiwemo salfa ambavyo vinaweza kusababisha vifo kwa nyuki wakati wanakwenda kwenye maua kutafuta chavua.
Balozi Dkt. Batilda Buriani alitoa kauli hiyo leo wakati akihutubia kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Alisema asali ni nembo ya kielelezo kikubwa cha Mkoa wa Tabora kwa hiyo shughuli yoyote ya kuathiri makundi ya nyuki si vema ikafanyika.
Balozi Dkt. Batilda aliongeza kuwa nyuki wanazofaida nyingini ikiwemo uchavushaji mimea ya mazao mbalimbali na uzalishaji wa asali na mazao mbalimbali ya nyuki.
Balozi Dkt. Batilda alisema vitendo vya kuhatarisha maisha yao vinahatarisha pia maisha ya wakazi wa Tabora kwa kupoteza uatijiri wa asili wa asali na kuzodhfisha uzalishaji wa mazao mashamabani.
Alisema kimsingi hapingi ulimaji wa Korosho katika Mkoa huo bali kinachotakiwa kuangaliwa kwa upana faida na hasara zitakazopatikana kutokana na matumizi ya viwatilifu kwenye korosho dhidi ya uzalishaji wa asali.
Balozi Dkt. Batilda alisema ni vema watafiti wa wadudu na wale wa kilimo wakashirikiana ili kuja na msimamo wa aina moja katika suala la kilimo cha korosho Mkoani Tabora.
Alisema Mkoa huo uko katika mkakati mkubwa wa kuongeza matumizi ya mizingira kisasa ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa vitendo vya kuhatarisha maisha ya nyuki vitawarudisha nyuma.
Aidha Balozi Dkt. Batilda alisisitiza kuwa yapo mazao mengi ya kudumu nje ya korosho kama vile michikichi ambayo yakimwa Mkoani humo haya athari kwa nyuki.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa