Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kakola, unaogharimu shilingi milioni 603.8 fedha kutoka Program ya SEQUIP, uliopo Kata ya Kakola,Wilayani Tabora, na kuridhishwa na usimamizi wa mradi huo hususani kwa hatua nzuri zilizokamishwa.
Dkt. Batilda amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutoa fedha ambazo zimekamilisha mradi huo mkubwa na wenye viwango.
“Niendelee kuungana nanyi kumshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kutuletea fedha ambazo zimekamilisha mradi huu mkubwa” Alisema Dkt. Batilda
Sambmba na hilo Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto shule ili kufaidike na uwekezaji unaofanywa na Serikali.
“Kama mnavyoona serikali imeendelea kujenga shule mpya, na nyinyi kama wazazi au walezi hakikisheni mnawapeleka watoto shuleni” aliongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa
Pia, Mhe. Batilda amewataka Wasimamizi wa shule hiyo kuhakikisha suala la chakula mashuleni linatiliwa mkazo ili watoto waweze kupata chakula wakiwa shuleni. Sambamba na ujenzi wa matenki ya ardhini ili kuhakikisha maji ya mvua yanakusanywa hasa kwa kipindi hiki.
“nipende kuwasisitiza wasimamizi wote wa mradi huu, kuhakikisha wanatilia mkazo suala la chakula shuleni ili watoto wapate chakula wakiwa shuleni” Alisisitiza Mhe. Batilda
Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mhe. Peter Bura, na watendaji wote wa wilaya kwa kusimamia vema mradi huo ambao kwa kuzingatia ubora unaotakiwa.
“Kwa hakika Mhe. DC umefanya kazi Kubwa sana, nipende kutoa pongezi zangu kwako, watendaji na kamati nzima ya ujenzi pamoja na wananchi wote” alisema Mhe. Mkuu wa Mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akikagua miundombinu ya madarasa yenye ubora yaliopo kwenye mradi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kakola uliopo Kata ya Kakola, Wilayani Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akikagua maabara ya kisasa na yenye ubora iliyopo kwenye mradi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kakola uliopo Kata ya Kakola, Wilayani Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akipata Maelezo kutoka kwa msimamizi wa mradi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kakola uliopo Kata ya Kakola, Wilayani Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akikagua ubora wa madiisha yaliotumika katika mradi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kakola uliopo Kata ya Kakola, Wilayani Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Peter Bura akitoa ufafanuzi mfupi na kisha kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian mara baada ya zoezi la ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kakola, uliopo Kata ya Kakola, Wilayani Tabora.
Diwani kata ya Kakola Mhe. Chota Charse akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi ambazo zinakamilisha mradi huu mkubwa na wenye viwango. Na pia amewashukuru viongozi kuanzia ngazi ya mkoa mpaka ngazi ya kata na kijiji kwa kuhakikisha mradi huo unajengwa katani hapo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kakola Ndugu. Kaunda Kipoya amempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha ambazo zimetumika kwenye mradi huu mkubwa ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kakola, Wilayani Tabora.
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Emmanuel Fashaho ameishukuru serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kujenga shule hii mpya ya Sekondari Kakola na kuwapumguzia changamoto ya umbali, ambapo awali wananfunzi walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 10.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Tabora Ndugu. Gudu Malulu amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, kusimamia suala la chakula shuleni, na tayari kumeshafanyika jitihada za awali kwa kuwashirikisha viongozi wa kata na vijiji ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na suala la chakula shuleni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandaliwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkuba, Ndugu. Boro Ndunguru imeeleza kuwa, mpaka kukamilika kwake mradi huu wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kakola utagharimu shilingi milioni 603.8. Ambapo kiasi cha shilingi milioni 551.1 kimeshatumika, na kiasi cha shilingi milioni 52.7 kimebakia, kupitia programu ya SEQUIP.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa