Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amefungua mafunzo ya siku tano (5) ya kuwajengea uwezo wajasiriamali katika masuala ya usimamizi wa biashara, uandaaji wa mipango ya biashara na utafutaji wa masoko, yaliodhaminiwa na taasisi zisizo za kiserikali ya MEDA na INSPIRE yanayoendelea kufanyika katika ukumbi uliopo katika Hotel ya JM, Manispaa ya Tabora, Februari 26, 2024.
Akitoa hotuba yake Mhe. Mkuu wa Mkoa amezipongeza taasisi ya MEDA na INSPIRE kwa kuuchagua mkoa wa Tabora kuwa miongoni mwa mikoa ambayo imefaidika na mafunzo hayo kwa wajasiriamali ambao wengi ni wanawake na wamekuwa wakifanya vizuri katika shughuri za uzalishaji. Na wataka wajasiriamali walioshiriki kwenye mafunzo hayo kuzingatia mambo yote yanayofundishwa ikiwa ni moja ya njia ya kujiendeleza katika shughuri za uzalishaji.
Aidha, kuelekea siku ya wanawake duniani, Mheshimiwa Batilda ametoa wito kwa watendaji wote ngazi ya halmashauri kuhakikisha kuwa kuwa na shughuri za kufanya kabla ya kufikia kilele cha maadhimisho Machi, 8, 2024.
Naye. Mkurugenzi Mtendaji kutoka INSPIRE Consultant Ltd Ndugu. Deogratius Mahangila amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa kuwa mgeni rasmi na kushuhudia ufunguzi wa mafunzo hayo na kwamba kupitia Taasisi ya INSPIRE mamia ya wajasiriamali watafaidika na mafunzo hayo.
Mafunzo haya ya siku tano (5) ya kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya usimamizi wa biashara, uandaaji wa mipango ya biashara na utafutaji wa masoko yanahusisha majasirimali kutoka wilaya zote za mkoa wa Tabora na yanatarajiwa kuhitimishwa mnamo Machi 1, 2024.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa