Mhe. Mkuu wa Mkoa amsema kuwa, malengo ya mafunzo hayi ni kuhimarisha ulinzi pamoja na mambo mengine ni kupima utayari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kukabiliana na mashambulio ya kigaidi katika maeneo yenye mikusanyiko ya Watu ikiwa ni wajibu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kuwa Wananchi wanakuwa salama dhidi ya tishio la aina yoyote la usalama lakini pia zoezi hili lililenga kuwashirikisha Wananchi hasa wanachuo wa chuo cha Ualimu cha Tabora kujua wajibu wao katika Ulinzi wa Nchi yao kwa kutoa taarifa pale wanapoona mambo hayapo sawa au kumshuku mhalifu katika maeneo yao.
Sambamba na hilo, Mhe. Batilda Burian ametoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Tabora kuwa jukumu la usalama wa Nchi sio la Vyombo vya Ulinzi na Usalama pekee bali ni jukumu lao pia . Na kuchukua jukumu la kujoa taarifa pale kunaonekana viashiria vya uhalifu kwenye maeneo yetu.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Tabora amevipongeza vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mkoani hapo vilivyoshiriki katika zoezi hilo na amewaasa kuendelea kufanya mafunzo kama hayo ili kuboresha utendaji kazi wao na hivyo kuhakikisha Usalama wa Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa