Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amekabidhi magari manne ya Kubeba Wagonjwa kwa Wakuu wa Wilaya ya Kaliua, Sikonge na Uyui, ikiwa ni moja ya kumalisha usambazaji wa magari ya wagonjwa 900 yenye thamani zaidi ya Shilingi Bilioni 29, yaliotolewa kwa Halmashauri zote hapa nchini kwa malengo ya kukuza huduma za Afya hasa huduma ya Mama na Mtoto. Na magari mawili ya jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora yaliotolewa kwa malengo ya kukuza suala la ulinzi Mkoani Tabora.
Akikabidhi magari Hayo manne kwa halmashauri ya Sikonge, Kaliua na Uyui na magari mawili kwa ajili ya jeshi la Polisi, Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wasimamizi wa magari hayo kuhakikisha magari hayo yanatumika katika matumizi yaliopangwa na si matumizi mengine kama kubeba madawa ya kulevya na vitu vingine visivyohitajika.
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sikonge na Kaliua Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakalia Mwansasu akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za kinunulia magari ya Wagonjwa manne, ambapo leo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameyakabidhi kwa wakuu hao wa Wilaya.
Akitoa neno la Shukrani, Mhe. Zakalia Mwansasu amehaidi kuyatunza na kuyalinda magari ya kubebea wagonjwa ili kuhakikisha thamani ya Fedha zilizotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia zinafanya kazi ipasavyo kwa maslahi ya watanzania.
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC), Ndugu Hassan Wakasuvi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kupitia Mkoa wa Tabora Mohamed Nassoro Hamdan akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi wakati wa hafla ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kukabidhi magari manne ya kubeba Wagonjwa kwa Wakuu wa Wilaya ya Sikonge, Uyui na Kaliua iloyofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi. Novemba 16, 2023.
Akitoa salamu za chama Ndugu. Mohamed Nassoro ameeleza kuwa, kama viongozi wa chama hawana budi kumshukuru Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa kikamilivu kwa hapa Mkoani Tabora na Tanzania kwa ujumla. Na kusema kuwa kupitia haya yanafanywa na Mhe. Rais yanatufanya sisi viongozi na wanachama kutembea kifua mbele.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi Magari mawili ya Polisi Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi wa Polisi Richard Abwao.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakalia Mwansasu funguo mbili za magari ya Kubeba Wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi ufunguo wa Gari la Kubeba Wagonjwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mhe. Rafael Lufungija aliyeambata na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Dkt. Rashidi Chuachua.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Wilaya, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Baadhi ya watumishi kutoka Ofiisi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya na wadau wa sekta ya afya walioshiriki kwenye hafla ya kukabidhi magari manne ya kubeba wagonjwa na magaro mawili ya jeshi la polisi.
Hafla ya kukabidhi magari manne ya kubeba wagonjwa na magari mawili ya Jeshi la Polisi imefanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi na kuhidhuriwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, wadau wa sekta ya Afya pamoja na watendaji kutoka ngazi ya Mkoa na Wilaya.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa