Februari 4, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amepokea maboksi 10 ya peni kutoka kampuni ya EZY CARD iliyoko na tawi lake hapa Mkoani Tabora inayojishughurishwa na huduma za kadi za matukio mbalimbali kwa Njia ya kieletronikini.
Akipokea maboksi hayo, Mhe. Mkuu wa Mkoa ameishukuru kampuni hiyo kwa kujitoa kwake kwa Jamii hususani wakati wa majanga.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya EZY CARD Ndugu. Jimmy Albert Haizer Amesema kuwa, licha ya kampuni hiyo kuwa changa, bado kulikuwa na haja ya kampuni hiyo kujitoa kwa Jamii hususani kwenye kipindi cha majanga.
Maboksi hayo kumi (10) yanatarijiwa kupelekwa kwa wanafunzi wa sekondari ya Ziba ambao Januari 23, 2024 waliunguliwa na vitu vyao kutokana na ajali ya kuungua moto bweni la wavulana lililopo shuleni hapo.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa