MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wito kwa Wakazi wa Igagala Wilayani Kaliua kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO -19 ili wawe salama katika Maisha yao.
Alisema chanjo ya UVIKO -19 ni hiari katika kuhakikisha kuwa mhusika anakuwa katika mazingira yakutoathirika na virusi vya CORONA.
Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo leo wakati wa mkutaano wa hadhara kwenye Kijiji cha Igagala wilayani Kaliua.
Alisema kwa wale ambao hawataki kuchanja wanajiweka katika hatari za kupata maambukizi na kuhatarisha Maisha ya watu wengine."Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassana anatupenda ndio maana ametuletea chanjo na yeye amechanja na Mimi kama Mkuu wenu wa Mkoa nimechanja na Mkuu wenu wa Wilaya amechanja ...watataalamu wamesema chanjo ni salama " alisisitiza
Balozi Dkt. Batilda alisema pamoja na kuchanja chanjo ya UVIKO -19 ni vema tahadhari zote za kujikinga ikiwemo kuvaa Barakoa , kunawa maji tirika , kukaa umbali unaoshauriwa na wataalamu wa sekta ya afya na kutumia vitakasa mikono.
Alisema kutokana na Mkoa wa Tabora kuwa na mwingiliano na wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya Tanzania tatizo la Corona lipo.
Balozi Dkt. Batilda alisema wagonjwa wapo ambao wengine wako katika hali ya kuhitaji mashine za kupumulia, wengine wako wamelazwa.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewataka Wakazi wa Igagala wilayani Kaliua kujiunga na Bima ya Afya ili wawe na uhakika na matibabu wakati wote.
Alisema mpango wa Serikali ni kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na Bima ya afya.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa