Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ameungana na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), katika kampeni ya upandaji wa miti kupitia kampeni ijulikanayo kama “Mti wa Mama” inayoendelea nchi nzima. Akiongea na wananchi baada ya kukamilisha zoezi la upandaji wa miti Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo yao na kwamba serikali itaendelea kupanda miti hasa katika maeneo ya taasisi ikiwemo shule na zahanati na kuhakikisha kuwa miti inayopandwa inatunzwa.
Ambapo kwa mkoa wa Tabora, tayari kumeshaanzishwa kampeni ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapanda mti na kila mtoto anayezaliwa pia atapanda mti ili kuhakikisha suala la utunzaji wa mazingira linakuwa la nchi nzima na kwa wananchi wote.
Kwa upande wake Mhifadhi Misitu TFS Mkoa wa Tabora Kamanda Aloyce Kilemwa amesema kuwa, kwa mwaka huu TFS imepanga kupanda miti laki sita na ishirini na tayari mpaka sasa miti laki tatu imeshapandwa, na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira na kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa kuunga mkono kampeni hiyo ya upandaji wa miti.
Naye, Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Tabora Ndugu. Ashura Mwazembe, ameipongeza serikali kwa kuanzisha kampeno hii ya upandaji wa miti ambayo imekuwa na tija kwa wananchi.
#TaborayaKijanikwaMaendeleayaTaifa
#TorontoyaUnyamwezini
#Tanzaniayakijani
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa