Serikali ya mkoa wa Tabora inatarajia kuwafikia watoto 544,616 wenye umri chini ya miaka mitano katika Kampeni ya chanjo ya Surua Rubela itakayoafanyika nchi nzima kwa siku siku nne kati ya February 15 na 18 mwaka huu.
Akizungumza na wadau wa afya mkoa Mganga Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa amesema mwaka 2019 kampeni kama hiyo ilipofanyika mkoani Tabora licha ya ripoti za ndani kuonesha walifikia watoto kwa asilimia zaodi ya 100 lakini baada ya uhakiki ilionekana mkoa umewafikia watoto kwa asilimia 62 na kwamba hawataki jambo hilo litokee mwaka huu.
Kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tabora, Mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo amesema wataalamu wa afya wazingatie maadili wakati wa uwasilishaji wa takwimu akiwataka kuwekeza kwenye elimu ili kuwafikia kwa wingi watoto wote waliokusudiwa badala ya kupika takwimu.
Aidha Mtondoo ameielekeza idara ya afya kutumia kampeni hii pia kutoa chanjo nyingine za watoto ambazo walizikosa huko.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa