• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

TABORA YAZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI

Posted on: May 10th, 2021

TABORA YAZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI

MKOA wa Tabora imezindua Kitabu cha mwongozo wa Uwekezaji unaonyesha fursa zilizopo ambazo zinaweza kuwasaidia Wawekezaji  kupata maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya  kuinua hali ya uchumi wa watu wa mkoa huu na Taifa kwa ujumla       

Mwongozo huo ulizinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Geofrey Mwambe katika ukumbi wa Mtemi Isike ulipo katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo mkubwa wa kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara ili kuvutia uwekezaji utakaoinua uchumi wetu.

Mwambe alisema mwongozo wa Mkoa wa Tabora umeonyesha utajiri na fursa nyingi zilizopo zikiwemo za maliasili, madini, mifugo, kilimo cha tumbaku, pamba, alizeti pamoja na shughuli za ujasiriamali mdogo na wa kati.

Aliongezea kuwa, zipo fursa mpya zinazojitokeza katika mkoa huu ambazo ni pamoja na bomba la mafuta ghafi linalotoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga na kupiti mkoa wa Tabora, ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, umeme wa REA, barabara za lami, Maji toka Ziwa Victoria na ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo cha aina mbalimbali.

Mwambe aliwataka Watendaji wa Serikali kuachana  na urasimu, na vikwazo visivyo na tija ambavyo vinawakwaza wawekezaji wanapofika katika Mkoa kuwekeza.

Aidha aliutaka uongozi wa Mkoa wa Tabora kuendelea kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji cha Kanda (TIC) kilichopo Kigoma kuanzisha Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja (One Top Centre) na kuhakikisha kinakuwa na rasilimali za kutosha.

Katika hatua nyingine Waziri huyo alisema kuwa wanaendelea na taratibu za kuchukua viwanda vilivyobinafishwa na havifanyi kazi kama vilivyokusudiwa kikewemo cha Kiwanda cha Nyuzi Tabora na kile cha Maziwa,

Alisema lengo ni kutafuta wawekezaji vingine ambao wataviendesha kwa tija kwa ajili ya kuongeza ajira na kuchochea uchumi wa Nchi.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Utatibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama alisema Mpango huu utawawezesha wakulima hususani vijana kupata pembejeo na masoko ya kuaminika ya bidhaa zao na kuhakikisha wanajikita katika kilimo biashara cha mashamba ya pamoja.

Alisema mpango wa kilimo cha mashamba ya pamoja (Block Farming) inaratibiwa na Wizara ya Kilimo kwa lengo la kuwawezesha wananchi hususani vijana kufanya kilimo biashara chenye tija na kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo.

Jenista alisema kupita kilimo cha pamoja vijana watawezeshwa kupata mbolea kwa urahisi, kupata pembejeo za kilimo, kuwekewa utaratibu mzuri na nafuu wa kusafirisha bidhaa zao kutoka shambani hadi sokoni na watawezeshwa kupata masoko ya uhakika ya bidhaa zao.

Alisema mfumo huo ukisimamiwa vizuri ndio njia sahihi itakayoiwezesha Tanzania kufanya mapinduzi katika Sekta ya Kilimo kwa kuwa unachochea matumizi ya teknolojia za kisasa na kuwezesha tija kubwa katika sekta ya kilimo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Dkt. Philemon Sengati  alisema uwepo wa mwongozo huo utasaidia kutangaza fursa na vivutio vya uwekezaji ikiwemo ardhi, idadi kubwa ya mifugo takribani milioni 3.7, utalii wa kihistoria, uwepo wa madini na mapori ya akiba pamoja na misitu ya hifadhi inayofaa kwa ufugaji wa nyuki na uvunaji wa mazao ya misitu.

“Zipo sababu nyingi za kuwekeza Tabora ikiwemo uhakika wa upatikanaji wa maji, uwepo wa barabara za lami zinazounganisha Tabora na Mikoa jirani, uwanja wa Ndege wenye njia mbili za kurukia ndege, uwepo reli iliyoboreshwa , umeme wa uhakika na uwepo wa maeneo ambayo yameshapimwa kwa uwekezaji,”alisema.

Mwongozo huo umetayarishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Mkoa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mwisho

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa