Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Urambo limepitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kiasi cha Bilioni 30.33, ambapo Mapato ya ndani ni kiasi cha Bilioni 4.2 na Tsh. Bilioni 26.0 ikiwa ni Ruzuku kutoka Serikali kuu pamoja na Wafadhili mbalimbali wa Maendeleo kwenye Kikao cha Baraza la kupitisha Bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo leo Februari 7, 2024.
Ili kukamilisha mpango wa bajeti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri (W) Bi.Grace Quintine amesema Halmashauri itahakikisha inakusanya Mapato yake ya Ndani kupitia miradi mbalimbali iliyoanzishwa kwa Asilimia mia moja (%100) kwa mwaka wa fedha 2024/2025
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe.Adam Malunkwi amemtaka Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha yeye na watalaamu wake wanakusanya mapato ya ndani ili vipaumbele vya Halmashauri vitekelezwe kikamilifu kama mpango wa bajeti ulivyopendekezwa.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji Bi. Grace Quintine amesema Bajeti itaelekezwa zaidi kwenye Miradi ya Maendeleo ikiwemo Elimu, Afya na Miundombinu.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa