• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

VIJIJI VYOTE VYA MRADI WA REA KUWA NA UMEME IFAKAPO DESEMA MWAKA HUU: DKT KALEMANI

Posted on: September 30th, 2019

VIJIJI VYOTE VYA MRADI WA REA KUWA NA UMEME IFAKAPO DESEMA MWAKA HUU: DKT KALEMANI

SERIKALI imetoa miezi mitatu kwa Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa  kabambe wa kusambaza umeme vijijini nchini awamu ya tatu (REA III) kuhakikisha wamekamilisha kuunganisha umeme katika vijiji vyote vilivyopo katika mradi huo ifikapo Desemba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme katika eneo la Mwambaha wilayani Nzega.

Alisema endapo itafika Desemba mwaka huu kazi haijakamilika itabidi Serikali ichukue hatua dhidi ya Mandarasi ambaye atakuwa hajaunganisha umeme katika Vijiji walivyokubaliana.

“Kwa vile Sasa hakuna changamoto ya vifaa kama vile nyaya, nguzo na transformer , ni matarajio yetu speed itakuwa kubwa na kuunganisha umeme katika vijiji mbalimbali…kwa hiyo tusingependa kuona Mkandarasi anakuwa mzembe kwa hatua yoyote ile…tukiona mkandarasi akuwa mzembe ni vema tuone ni hatuna gani tunachukua mapema badala  ya kusubiri hadi mwisho” alisisitiza.

Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha vijiji vyote vilivyo katika REA III vinafikiwa umeme , kazi itakayobaki ni kusambaza kwa mwananchi mmoja mmoja anayelipia umeme .

Aidha Dkt. Kalemani alisema Serikali imeagiza katika maeneo ambayo njia kuu za umeme zinapita na vitongoji na vijiji ambavyo havina umeme ,Shirika la Ugavi wa Umeme nchini(TANESCO)  kuhakikisha navyo vinapata umeme.

Katika hatua nyingine Serikali imetoa shilingi bilioni 2.5 kila Mkoa ili kuimarisha miundombinu ya usambazaji umeme nchini.

Dkt. Kalemani alisema fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa nguzo, nyaya na ‘transformer’ ili kuzuia kukatikati kwa umeme mara kwa mara hapa nchini na kusaidia wananchi kuwa na fursa za kufungua njia kubwa za uchumi na ujenzi wa viwanda.

Wakati huo huo Waziri wa Nishati amewataka wananchi ambapo umeme tayari umefika kuchangamia fursa za mradi wa REA III ili waweze kuunganisha umeme ili uwasidie kuanzisha viwanda vidogo vidogo ikiwemo vya kusindika mazao kwa ajili ya kuyaongezea ubora.

Alisema upatikanaji wa umeme utawasaidia kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kiusalama na hivyo ni vema wakachangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Serikali.

 

 

 

Mwisho

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa