• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

WADAU TUSHIRIKIANE KATINA KUBORESHA ELIMU NCHIN-NZUNDA

Posted on: July 29th, 2019

WADAU TUSHIRIKIANE KATINA KUBORESHA ELIMU NCHIN-NZUNDA

SERIKALI imetoa wito kwa wadau wa elimu kushirikiana na Serikali katika kujenga mazingira mazuri ya utoaji wa elimu nchini ikiwemo ujenzi wa madarasa, vyoo na nyumba za walimu.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Mwanza na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kuandaa vipindi vya redio kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE-Tanzania)

Alisema hali ilivyo sasa ili kukamilisha miundombinu na kuweka mazingira mazuri ya utaoji wa elimu na ujenzi wa nyumba za kuishi walimu zinahitajika shilingi trilioni 14 kutekeleza zoezi hilo katika Shule za Sekondari na Msingi nchini kote.

Nzunda alisema Serikali pekee yake haiwezi kukamilisha zoezi hilo bila kushirikiana na wadau wengine ili kujenga madarasa ya kutosha ili kupunguza msongamano wa wanafunzi, kuondioa uhaba wa nyumba za walimu na vyoo.

Alisema Serikali katika kukabiliana na tatizo la msongamano wa wanafunzi katika shule mbalimbali za Msingi na Sekondari tayari katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita imetoa zaidi ya bilioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa maboma ya madarasa 5,289  nchini kote.

Nzunda alisema kuwa  fedha hizo zimesaidia kukamilisha maboma 2,392 kwa ajili ya Sekondari  na 2,897 ni kwa ajili ya Msingi nchini kote.

Aidha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) -  anayeshughulikia Elimu aliwataka wadau wa elimu ikiwemo

Alisema kuwa badala ya Asasi zisizo za Kiserikali(NGOs)  kutumia fedha katika utetezi(advocacy) unaonyesha na kutangaza changamoto na mapungufu katika Shule nchini kama vile msongamano na upungufu wa matundu ya vyoo mashuleni ni vema wakatumia fedha hizo kushirikiana na Serikali katika kuboresha mazingira ya Shule nchini.

Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) -  anayeshughulikia Elimu amepiga marufuku kwa walimu wanaofundisha  madarasa ya kuanzia elimu ya awali hadi darasa la tatu kuingia na viboko madarasa.

Alisema kuwa vitendo hivyo vinasababisha wanafunzi wa madarasa hayo kuogopa na kutokuwa wasikivu wakati wa wanapofundishwa.

Kuhusu Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE-Tanzania) alisema kuwa umechangia katika kuboresha elimu katika mikoa 9 kiwango cha ufaulu kwa shule za Msingi umeongezeka kutoka chini asilimia  40 hadi kuwa  juu ya 77 na maeneo mengine kufikia asilimia  100.

Mafunzo hayo ya siku tatu kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE-Tanzania) yanayowashirikisha waandishi wa habari, Maafisa Elimu Mikoa na Maafisa Habari kutoka Mikoa 9 yameandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza(DFID)

 

 

MWISHO

 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa