Wizara ya Katiba na Sheria imeendesha mafunzo maalum kwa wataalam ngazi ya mkoa na halmashauri kwa ajili ya kuwandaa kwenda kuwahudumia wananchi wa mkoa wa Tabora katika kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya mama samia ijulikanayo kama Mama Samia Legal Aid Campaign.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Bi. Jane Lyimo amesema baada ya mafunzo hayo ni matarajio ya serikali kuwa wananchi watakwenda kuhudumiwa kwa ufanisi mkubwa hasa kuwafikia wananchi wasio na uwezo na waishio pembezoni ambako msaada wa kisheria haupatikani kwa urahisi au kwa sababu ya kushindwa kumudu gharama ya kukodisha wakili au wale walio mbali na maeneo ambapo msaada wa kisheria haupatikani kabisa.
“Ni imani yangu kuwa maarifa na ujuzi utakaopatikana katika mafunzo haya,utawawezesha kutekeleza kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia kwa weledi na ujuzi na hivyo ni wasihi mafunzo haya yawe ni chachu kabisa na mwangaza wa kuwasaidia wananchi wakati wa utoaji wa msaada wa kisheria katika kipindi hiki cha kampeni”. Ameeleza.
Kwa upande wao watalaam waliohudhuria mafunzo hayo wameishukuru serikali kwa zoezi hili adhimu litakalo kwenda kuisaidia jamii na kuahidi kwenda kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata miongozo iliyotolewa na wizara ya sheria na katiba.
Masuala yatakayoanganziwa na kampeni ya msaada wa kisheria ya mama samia ni pamoja na haki za binadamu ,utawala bora,mirathi,wosia,madai pamoja na jinai.Kampeni hii ya msaada wa kisheria inaongozwa na kauli mbiu isemayo “Msaada wa Kisheria kwa Haki,Usawa,Amani na Maendeleo”.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa