Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko amewasili Mkoani Tabora kwa ajili ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu (3) ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, kutembelea taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) na mwisho kushiriki kwenye uzinduzi wa mafunzo ya kutengeneza nyuzi na vitambaa kutoka zao la pamba kwa teknolojia na walimu kutoka Indonesia
Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko akiwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na kupokelewa na Mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian leo Machi 2, 2024.
Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya pili Ndugu. Ally Hassan Mwinyi aliyefariki siku ya jana Februari 29, 2024.
Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko akiongoza dua fupi mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya pili Ndugu. Ally Hassan Mwinyi aliyefariki siku ya jana Februari 29, 2024.
Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian mara baada ya kuwasili Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Tabora Machi 2, 2024
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko mara baada ya viongozi hao kuwa na mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi mdogo uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora leo Machi 2, 2024
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian mara baada ya viongozi hao kuwa na mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi mdogo uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora leo Machi 2, 2024
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimuonesha Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko baadhi ya bidhaa zitokanazo na pamba, zilizozalishwa na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA kilichopo Manispaa ya Tabora, mara baada ya viongozi hao kuwa na mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi mdogo uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora leo Machi 2, 2024
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian mara baada ya viongozi hao kuwa na mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi mdogo uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora leo Machi 2, 2024
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa