Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Kamati ya Bunge ya Kupambana na Masuala ya Malaria na Wataalamu kutoka OR- TAMISEMI na Wizara ya Afya wakiwasili Wilayani Uyui na Kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakalia Mwansasu, kwa ajili ya ziara ya siku moja ya Kutembelea mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Uyui Novemba 14, 2023.
Mhe. Zakalia Mwansasu akiwakaribisha na kutoka taarifa ya Wilaya kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI na Kamati ya Bunge ya Kupambana na Masuala ya Malaria na Wataalamu kutoka OR- TAMISEMI waliofika Ofisi Kwake kwa ajili ya ziara ya siku moja Wilayani humo ambapo watatembelea mradi wa Hospitali ya Wilaya .Novemba 14, 2023.
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakalia Mwansasu, Dkt Joseph Welema akisoma taarifa ya Wilaya kuhusiana na utolewaji wa huduma ya Mama Na Mtoto pamoja na Huduma za Kudhibiti Malaria katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Baadhi ya Wabunge wakichangia taarifa ya Wilaya kuhusiana na utolewaji wa huduma ya Mama na Mtoto pamoja na Huduma za Kudhibiti Malaria katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui iliyowasilishwa na Dkt. Joseph Welema kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Zakalia Mwansasu.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Kamati ya Bunge ya Kupambana na Masuala ya Malaria na Wataalamu kutoka OR- TAMISEMI na Wizara ya Afya wakiwasili katika hospitali ya Wilaya ya Uyui ambapo walipata taarifa na kufanya ukaguzi wa mradi huo.
Tumaini Fumbuka Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Uyui akisoma taarifa ya Hospitali ya Wilaya ya Uyui kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Kamati ya Bunge ya Kupambana na Masuala ya Malaria na Wataalamu kutoka OR- TAMISEMI na Wizara ya Afya mara baada ya kuwasili hospitalini hapo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Kamati ya Bunge ya Kupambana na Masuala ya Malaria na Wataalamu kutoka OR- TAMISEMI na Wizara ya Afya wakitembelea, kukagua na kujionea kazi na huduma mbalimbali zinazotolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui.
Ambapo Wajumbe wa kama hizo wametoa maoni, mapendekezo na ushauri kwa watalaamu na wasimamizi wa hospitali ya Wilaya ya Uyui ili kuhakikisha huduma bora za afya hususani katika suala zima la huduma ya Mama na Mtoto na Malaria zinatolewa kwa wananchi wa Uyui na Tabora kwa ujumla.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Kamati ya Bunge ya Kupambana na Masuala ya Malaria na Wataalamu kutoka OR- TAMISEMI na Wizara ya Afya wakifanya majumuhisho ya ziara yao ya kikazi Wilayani Uyui ambapo walitembelea Hospitali ya Wilaya na kutoa mapendekezo kama Matumizi ya mifumo ya kisasa, Uandaaji bora wa taarifa za Serikali, Watendaji kuweka mipango mipya ya kukabiliana na Malaria na pia kuwa na ubunifu katika utendaji wa kazi.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Kamati ya Bunge ya Kupambana na Masuala ya Malaria na Wataalamu kutoka OR- TAMISEMI na Wizara ya Afya walifika na kuanza ziara yao Novemba, 13, 2023 ambapo walitembelea Hospitali ya Rufaa ya Kitete na kufikia tamati leo Novemba 14, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa